NIGERIA YAFUNGWA 2-1 NA URUGUAY KOMBE LA MABARA



nigeria f78bf
John Obi akishangilia bao
  
nigeria2 fb813
Forlan akichangilia na wenzake
MSHAMBULIAJI Diego Forlan usiku wa kuamkia leo amesherehekea mechi yake ya 100 Uruguay kwa kufunga bao la ushindi timu yake ikishinda 2-1 dhidi ya Nigeria kwenye Kombe la Mabara mjini Salvador.

Forlan alifunga mwanzoni mwa kipindi cha pili baada ya John Obi Mikel kuisawazishia Nigeria dakika ya 37 kufuatia Uruguay kufunga bao la kuongoza dakika ya 19 kupitia kwa Diego Lugano.
Matokeo hayo yanafanya timu mbili katika Kundi hilo, B zilingane kwa pointi, tatu kila moja baada ya kucheza mechi mbili, lakini ikiwa imebakiza mechi na Tahiti, Uruguay iko katika nafasi kubwa ya kusonga mbele pamoja na Hispania, yenye pointi sita na itacheza na Nigeria katika mechi ya mwisho ya kundi hilo.
Previous Post Next Post