Muigizaji wa Bongo Movie Jaji Khamis aka Kashi afariki dunia



Muigizaji wa filamu nchini Jaji Khamis (Kashi) amefariki dunia mchana huu katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.


Kashi amewahi kutamba na mchezo wa ITV, Tamu Chungu akiwa na wasanii wenzake kama Mzee Masinde,Samson na wengine.

Baada ya kupata habari hii, Bongo61 imeongea na muigizaji mwenzake Monalisa ambae amethibitisha kutokea kwa msiba huo. Monalisa amesema alipata taarifa jana kwamba Kashi amelazwa hospitali akiwa amezidiwa kiasi cha kushindwa kuongea na hivyo kushindwa kujua nini kilikuwa kinamsumbua.

Naye Hemedy PHD ametweet: REST IN PEACE MUIGIZAJI MWENZETU JAJI KHAMIS KASHI….MUNGU AKULAZE PEMA PEPONI…MOVIE YA MWISHO TULICHEZA WOTE ILIKUA MATILDA!!Sad newz
Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA