Kevin Durant awa star wa kwanza wa NBA kusaini mkataba na Jay-Z kama wakala wake rasmi kupitia Roc Nation Sports


Baada ya kuidhinishwa kuwa wakala rasmi wa wachezaji wa mpira wa baseball (MLB) pamoja na basketball (NBA), Shawn Corey Carter aka Jay-Z kupitia Roc Nation Sports amesain mkataba wa kuwa wakala rasmi wa star wa NBA Kevin Durant.
kevin-durant-instagram
Mchezaji huyo star wa timu ya mpira wa kikapu Oklahoma City Thunder (OKC), Durant ameshare picha kupitia instagram ikimuonesha akidondoka wino katika mkataba wake na Roc nation Sports ya Jay-Z.
Walioishatangulia kuwa familia ya Roc Nation Sports ni Robinson Cano wa New York Yankee na Geno Smith wa NY Jet.
Previous Post Next Post