Kajala Aamua Kunyoa Kipala.. Unajua Kisa na Mkasa soma Hapa



KAJALA

Mwigizaji aliyerudi uraiani hivi karibuni Kajala Masanja amefanya mabadiliko makubwa ya mtindo wake wa nywele baada ya kunyoa kipara “kikavu” kichwani mwake.

Katika picha alizozitoa mwigizaji huyo kupitia kwenye mtandao leo jioni, mwigizaji huyo ameonekana akiwa na kipara tofauti na alivyozoeleka na nywele nyingi siku za nyuma.

Bongo61 tuliamua kumtafuta mwanadada huyu ili kujua “kunani”?? na staili hiyo na tulimpigia simu na maongezi yalikuwa kama ifuatavyo:

Bongo61: Mambo kajala, mzima?

Kajala: Mzima, kwema?

Bongo61: Kwema kabisa, vipi tena na kipara kichwani?

Kajala: Aha,..Siunajua tena mishe mishe, nipo na shoot movie yangu mpya ndo mana imenibidi ninyoe kipara maana inanilazimu kuonekana hivyo ndani na Filamu hiyo.

Bongo61: Okay, na itaitwaje?

Kajala: Itaitwa Heart attack

Bongo61: Umewashirikisha nani na nani humo ndani?

Kajala: Atakuwepo Hemedi na mastaa wengine Kibao, kifupi ni bonge la movie yaani usiipimie kabisa.

Bongo61: Basi tunaisubiri kwa hamu sana

Kajala: Pamoja sana.
Previous Post Next Post