Tunaamini unaweza kuwa mmoja kati ya watanzania wengi wasiolifahamu jina la Ardo King. Ardo ni rapper aliyezaliwa jijini Dar es Salaam lakini alikulia Mwanza na ni wa kitambo sana.
Kitambo sana aliwahi kuhit na ngoma iliyoitwa ‘Nani Atabaki’ aliyeirekodi kwenye studio za Mwanza Records zilizokuwa chini ya producer mkongwe, Enrico wa Sound Crafters. Baada ya hapo Ardo aliendelea kutoa ngoma kadhaa alizorekodi kwenye studio za Dar es Salaam.
Kuna muda alikuwa akifanya kazi bandarini jijini Mwanza kabla ya kupata mchongo wa ‘green card’ kwenda kuishi na kufanya kazi nchini Marekani. Pamoja na kufanikiwa kimaisha, Ardo hakuzitupa ndoto zake za kuendelea kufanya kile akifanyacho kwa ubora (do what he does best) Hip hop.
Mwaka 2010 alifungua studio yake kwao Mwanza aliyoipa jina la One Love (studio ambayo inaendelea lakini chini ya umiliki wa producer Tiddy Hotter ikiitwa One Love FX).
Ardo King alifanikiwa kujiimarisha zaidi kwenye hip hop ili kwendana na rap ya Marekani kwa ‘upgrade zaidi swag’ na kuanza kufanya hip hop kwa Kiingereza. Hiyo imelifanya jina lake liyakune masikio ya wadau wa muziki huo jijini Chicago na kuanza kupewa mashavu ya kupanda kwenye stage za show kadhaa kama tangazo hili la show ya hivi karibuni jijini humo linavyosikika likimtaja.
Hivi karibuni, Ardo aliachia single yake mpya na kali iitwayo ‘All I have’ aliyomshirikisha mwanadada Passion na tayari ameshafanya video ya ngoma hiyo itakayotoka hivi karibuni.
Tazama picha za utengenezaji wa video yake ya All I Have.