HISPANIA NA BRAZIL FAINALI KOMBE LA MABARA, YAING'OA ITALIA KWA MATUTA


10 4fab9
 Wachezaji wa Hispania wakishangilia ushindi

20 3025f


30 bc3d3

40 9169e

50 a6bb2

60 57414

70 eed5d

HISPANIA imeitoa Italia katika Kombe la Mabara kwa ushindi wa matuta wa 7-6 mjini Fortaleza, kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 120 katika mchezo wa Nusu Fainali usiku huu.

Wataliano walifungwa na Waspanyola katika Fainali ya Euro mwaka jana wameshindwa kulipa kisasi na sasa Fainali ya michuano hiyo mwaka huu Jumapili Uwanja wa Maracana, itawakutanisha wenyeji La Roja na Brazil wenyeji.
Leonardo Bonucci wa Italia alikosa moja ya penati 14 na Jesus Nevas akaweka nyavuni mkwaju wa mwisho kwa upande wa Hispania.
Si zaidi ya mwaka uliopita, Italia walipigwa 4-0 mjini Kiev, lakini The Azzurri waliwasili Fortaleza wakiamini kisasi kinawezekana, ingawa haikuwa hivyo.
 

Mikwaju ya penalti;  Jesus Navas alifunga a ushindi na kufanya 7-6 , baada ya Leonardo Bonucci mkwaju wake kuota mbawa.
 

Wengine wote waliotangulia walifunga; upande wa Hispania ni Sergio Busquets,  Juan Manuel Mata,  Sergio Ramos, Gerard Pique, Andries Iniesta na Hernandez Xavi.
Italia ni Riccardo Montolivo, Andrea Pirlo, Sebastian Giovinco, Daniele De Rossi, Alberto Aquilani na Antonio Candreva. 

-----------------------------
news via: : binzubeiry
----------------------------
Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA