Filamu ya Aunt Ezekiel yazuiwa kuingia sokoni kwa kukosa maadili. Bodi ya filamu yamtaka airekebishe.



Filamu ya Scola ya mwigizaji Aunt Ezekiel imezuiwa kuingia sokoni na bodi ya Filamu Tanzania kutokana kuwa na “scene” zinasemekana kuwa kinyume na maadili ya Tanzania.
Filamu hii imegundulika kuwa ina matatizo hayo baada ya muigizaji huyo kuipeleka kwenye bodi hiyo ili ikaguliwe kabla ya kuingia sokoni
Kupitia rafiki wa karibu na staa huyo ambaye alifafanua kuwa rafiki yake (Aunt) amekaliwa kooni na bodi hiyo lakini bado yupo katika mazungumzo kuona kama anaweza kuruhusiwa aendelee.
“Amejaribu kuwasihi ili kama kuna uwezekano iingie mtaani pasipo kuviondoa hivyo vipande kwani navyo vina umuhimu wake,” alisema rafiki huyo wa Aunt.

Alipotafutwa Aunt kuhusiana na suala hilo, alikiri kukaliwa kooni na bodi na kuomba apewe muda wa siku mbili ili aweze kulitolea ufafanuzi suala hilo lakini hakufanya hivyo, badala yake akasafiri nje ya nchi.
Mwaka jana mwishoni, bodi hiyo ya filamu ilimzuia mwigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ kuingiza sokoni sinema ya Sister Mary baada ya kuridhishwa na madai ya Kanisa Katoliki yalioainisha kuwa asilimia kubwa vipande vya sinema hiyo vilidhalilisha Ukatoliki.

--------------------------------
news via:  Global Publishers
--------------------------------------
Previous Post Next Post