Shughuli hii yatazamiwa kufanyika katika ukumbi wa Mlimani City ulipo jijini Dar es Salaam kuanzia saa moja usiku.yatakayokuwemo ndani ya Mlimani City ni pamoja na chakula cha jioni watakaokaa VIP na vitafuno kwa watakaokaa kawaida.Utoaji tuzo unatazamiwa kuanza saa tatu kamili.
‘Zoezi la red carpet linatazamiwa kuanza saa moja kamili hadi saa mbili jioni ambapo chakula kitaanza mpaka saa tatu kamili shughuli itakapoanza”. Alisema Bwana Kavishe.
Tiketi zitaanza kuuzwa kuanzia jumanne june 4, 2013 katika ukumbi wa Mlimani City Hall,Born to Shine Mwenge,Roby one Fashion Kinondoni na Sharks Limited Mtoni kwa Azizi Ali karibuni na Equator. “Naomba kusisitiza kwa Ticket za VIP zitauzwa ukumbi wa Mlimani City pekee na ziko chache sana kwahivi nawasii wale watakaopenda kuhudhuria mnunue ticket zenu mapema.” Alimaliza Geogre Kavishe.
Kwa mwaka huu shughuli ya mlimani city itaonyeshwa live na ITV na pia ili kuzisogeza tuzo kwa wananchi tumechagua mikoa michache ambapo zitonyeshwa kwenye sreens
Kubwa katika maeneo tofauti katika mikoa mitatu.Sehemu hizo kuwa ni Mwanza eneo la Mabatini, Temeke Uwanja wa Taifa na Kilimanjaro CCM Mkoa.
Kavishe alisema zoezi la kupigia kura wasanii kuelekea tuzo hizo zinazokwenda na kaulimbiu ya Kikwetukwetu mwaka huu lilifungwa Mei 31, mwaka huu.
Kuhusu burudani katika usiku huo, Kavishe alisema kwamba wasanii wa sasa wataimba nyimbo za wasanii wa zamani na wasanii wa zamani wataimba nyimbo za wasanii wa sasa.
“Kutakuwa na kitu tofauti sana upande wa burudani, ambacho kitapendeza na kuvutia sana, kwa ujumla maandalizi yako vizuri na tunatarajia mambo mazuri siku hiyo,”alisema Kavishe.