Drake atoa nyimbo 2 kwa mpigo, na tarehe ya kuachiwa album yake mpya 'Nothing Was The Same' yafahamika (Audio)



Siku chache baada ya rappers Kanye West na J.Cole kudondosha album zao ,Yeezus, na 'Born Sinner', na ikiwa zimebaki siku chache kabla Hova hajadondosha album yake mpya 'Magna Carta Holy Grail”, rapper kutoka Toronto, Canada Aubrey Drake Graham naye ametangaza tarehe rasmi ya kuachia album yake mpya 'Nothing Was The Same'.


Kupitia website yake ya OVOSound Drizzy ametangaza (September 17 ) ndio tarehe rasmi ya album yake kutoka.
Ikiwa kama sehemu ya kuwaandaa mashabiki wake Drizzy ameamua kutoa nyimbo 2 mpya kwa mpigo, ambazo ni Jodeci Freestyle” aliyomshirikisha J. Cole pamoja na “The Motions” featuring Sampha.
Zisikilize hapa


Previous Post Next Post