WESTMINISTER ABBEY WAIOMBEA TANZANIA





Urban Pulse Creative inakuletea taswira kutoka Westminister Abbey jijini London katika misa maalum ya kuombea amani nchi yetu ya Tanzania siku ya muungano iliyofanyika ijumaa tarehe 26.4.13.


Balozi wetu Mh Peter Kallaghe, maofisa kutoka ubalozini na baadhi ya watanzania waishio nchini Uingereza walijumuika pamoja kuhudhuria ibada hii maalum na raia wengine kutoka nchi mbalimbali. Ibada ilianza kwa jumuiya ya Abbey kuwaombea watanzania wote, viongozi pamoja na wanadiplomasia wote waliopo duniani na kwa ajili ya kazi maalum ya Ubalozi wetu hapa nchini Uingereza.


MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WABARIKI WATANZANIA


Asanteni,


Urban Pulse Creative
Mh Balozi Kallaghe akisalimia na Kiongozi wa kanisa baada ya ibada.
Bendera yetu ikipepea.
Kanisa la Westminister Abbey London.
Kutoka kushoto Abu Faraji, Caroline Chipeta, Mirium Mungula na mdau baada ya ibada.
Wazee wa kazi.
Picha ya Pamoja.
Previous Post Next Post