WAZIRI MKUU PINDA APOKEA MATEMBEZI YA MSHIKAMANO YA KUPAPAMBANA NA UWIZI WA KAZI ZA SANAA MJINI DODOMA LEO.









Waziri Mkuu Pinda akiwa katika picha ya pamoja na na baadhi ya Watangazaji wa Clouds FM (wote waliosimama nyuma).Reedio Clouds FM imezindua msimu wake mpya ulioitwa TWENZETU kwa minajili ya kuielimisha jamii kuwa na tabia ya kupenda vya kwao na kutumia fursa walizonazo ndani ya MADE IN TANZANIA kujikwamua kimaisha.
Waziri Mkuu Pinda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasaniii (wote waliosimama nyuma),mara baada ya kuzungumza nao kuhusiana na mambo mbalimbali juu ya sanaa ya Tanzania na namna ya kupambana na maharamia wa kazi zao,ambapo pia redio ya Clouds FM imezindua msimu wake mpya ulioitwa Twenzetu kwa minajili ya kueilmisha jamii ya kupenda vya kwao kutumia fursa walizonazo ndani ya MADE IN TANZANIA .
Waziri Mkuu Pinda akizungumza mbele ya baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya/Filamu pamoja na watangazaji wa Clouds FM na wadau wengine wa sanaa waliojumuika kwa pamoja kwenye tukio hilo adhimu kabisa mapema leo mchana,mara baada kufanyika Matembezi ya mshikamano ya kuitaka Serikali iendelee kuzilinda fursa zilizopo na pia kuendelea kuutanua wigo wa upatikanaji wa fursa hizo kwa wasanii na vijana wenyewe,ikiwa sambamba na kupinga uwizi/uharamia wa kazi za sanaa hapa nchini.


Mh.Pinda aliishukuru kampuni ya Clouds Media Group kwa kazi nzuri walioianzisha ya kuwasaidia vijana kwa namna moja ama nyingine katika suala zima la kuwaamsha na kuwafungua macho na kuwaelimisha namna ya kuziona fursa zilizopo kwa ajili ya kujikwamua kimaisha,aliongeza kuwa kupitia ujumbe huo wa MADE IN TANZANIA kinachohitajika sasa ni kupanga ratiba nzuri ya kuliendeleza zoezi hilo ikiwemo pia kwa kuzishirikisha taasisi nyingine zikiwemo za serikali katika kuhakikisha jambo hilo linaendelea.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Dkt.Rehema Nchimbi akiwakaribisha watu wote waliofika kwenye viwanja vya Nyerere Skwea,tayari kwa kumpokea mgeni rasmi,Waziri Mkuu Pinda.

Baadhi Wadau wa Muziki na Filamu wakiwa na mabango yao yaliyobeba jumbe mbalimbali mapema leo kwenye Matembezi ya mshikamano ya kuitaka Serikali iendelee kuzilinda fursa zilizopo na pia kuendelea kuutanua wigo wa upatikanaji wa fursa hizo kwa wasanii na vijana wenyewe,ikiwa sambamba na kupinga uwizi/uharamia wa kazi za sanaa hapa nchini,yaliyoanzia kwenye uwanja wa Jamhuri na kufikia tamati viwanja vya Nyerere Skwea 

Sehemu ya umati wa watu ukiwa kwenye Matembezi ya mshikamano ya kuitaka Serikali iendelee kuzilinda fursa zilizopo na pia kuendelea kuutanua wigo wa upatikanaji wa fursa hizo kwa wasanii na vijana wenyewe katika nafasi ya kujikwamua kimaisha,ikiwa sambamba na kupinga uwizi/uharamia wa kazi za sanaa hapa nchini,yaliyoanzia kwenye uwanja wa Jamhuri na kufikia tamati viwanja vya Nyerere Skwea 
Baadhi ya Wasanii wa Filamu hapa nchini Wema Sepetu sambamba na shosti yake Kajala walikuwa ni miongoni mwa wasaani waliounga mkono matembezi hayo ya mshikamano yaliyokuwa yametawaliwa pia na mabango kadhaa yaliyobeba jumbe mbalimbali za kupinga wizi wa kazi sanaa.



Matembezi ya mshikamano ya kuitaka Serikali iendelee kuzilinda fursa zilizopo,ikiwa sambamba na kupinga uwizi/uharamia wa kazi za sanaa hapa nchini . 
Baadhi ya magari yakiwa yamesimama yakipisha matembezi ya mshikamano yaliyokuwa yakielekea kwenye viwanja vya Nyerere Skwea mapema leo mchana.
Baadhi ya Watangazaji wa clouds FM,sambamba na wasanii wa muziki wa kizazi kipya/tasnia ya filamu na wadau wengine wa sanaa wakiwa wamejumuika kwa pamoja kwenye viwanja vya Nyerere Skwea mapema leo mchana,tayari kwa kumpokea mgeni rasmi,Mh Waziri Mkuu Pinda.
Mmoja wa Watangazaji wa kipindi cha Jahazi,Wasi Wasi Mwambulambo akiserebuka na Mh.Rehema Nchimbi.
Baada ya muda kulipita burudani ya pamoja ya mchanganyiko kama hivi safi kabisa kabla ya Waziri Mkuu kuwasili viwanjani hapo.
Pichani kati ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Rehema Nchimbi,kulia mtangazaji wa Clouds FM Mbwiga Mbwiguke na Shaffih Dauda (shoto) wakitwibiwirika kwa pamoja mapema leo mchana mjini Dodoma kwenye viwanja vya Nyerere skwea.
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni na Mdau mkubwa wa sanaa hapa nchini,Mh.Idd Azan akiunga mkono harakati za kupapambana na maharamia wa kazi za sanaa hapa nchini
Gari ya Waziri Mkuu Pinda ikiwasili
Waziri Mkuu Pinda akisalimiana na Naibu Waziri wa Habari,Vijana, michezo na Utamaduni,Mh.Amos Makala habari,Michezo mara alipokuwa akiwasili kwenye viwanja vya Nyerere Skwea mapema leo mchana mjini Dodoma. 
Waziri Mkuu Pinda akisalimiana na Mkurugenzi wa Vipindi na utafiti wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba mara alipokuwa akiwasili kwenye viwanja vya Nyerere Skwea mapema leo mchana mjini Dodoma.
Waziri Mkuu Pinda akiwasili kwenye viwanja vya Nyerere Skwea,mjini Dodoma mapema leo mchana huku akiwapungia mkono baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya/Filamu pamoja na watangazaji wa Clouds FM na wananchi wengine kwa ujumla waliojumuika kwa pamoja kwenye tukio hilo adhimu kabisa mapema leo mchana,mara baada kufanyika Matembezi ya mshikamano ya kuitaka Serikali iendelee kuzilinda fursa zilizopo na pia kuendelea kuutanua wigo wa upatikanaji wa fursa hizo kwa wasanii na vijana wenyewe,ikiwa sambamba na kupinga uwizi/uharamia wa kazi za sanaa hapa nchini,pichani kati ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Dkt.Rehema Nchimbi akimkaribisha. .
Mh.Waziri Mkuu Pinda akizungumza jambo na Muimbaji mahiri wa mashairi hapa nchini,Mrisho Mpoto.Kulia ni Mkurugenzi wa Vipindi na utafiti wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Chamwino,Mh.Fatma Ally akishuhudia mazungumzo hayo.
Previous Post Next Post

Popular Items