WADAU WA MUZIKI KUKUTANA LEO [MAY 29] LEADERS CLUB KWA AJILI YA MIPANGO YA KUISAIDIA FAMILIA YA MAREHEMU



Wadau wa muziki, wasanii pamoja na wote walioguswa na msiba wa Cowbama wanatarajia kukutana leo (May 29) saa 10 jioni katika viwanja vya leaders, kwa lengo la kuweka mipango mbalimbali ya ushiriki wa wadau wa burudani wakiwemo wasanii kwa ujumla katika kusaidia familia ya marehemu katika hatua zote za msiba na mazishi.


Akiongea na Bongo61 mmoja wa waratibu wa shughuli hiyo ya leo Dj Nicko Track wa Capital FM amesema wameshafanya mawasiliano na familia ya marehemu Mangwea na kuwa wamepanga kuwahusisha wana familia kwa hatua zozote zitakazochukuliwa na wadau hao baada ya kukutana leo.

Dada wa marehemu aitwae Evelyn amethibitisha kupata taarifa hizo “ wameniambia watakutana saa 10 wakishakutana saa 10 watanipa procedure zote zitakazokuwa zinaendelea kule”.

Kama wewe ni mdau wa muziki na shabiki wa Mangwea hii ni nafasi yako ya kushiriki katika msiba huu kwa kufika pale Leaders saa 10 jioni ya leo
Previous Post Next Post

Popular Items