Sunday, May 5, 2013

TIGO YAKUTANA NA KUSHEREHEKEA NA WAMILIKI WA BLOG

 Mmoja wa wawakilishi wa Kampuni ya Simu za mkononi ya tiGO, akizungumza na waamiliki wa magazeti tando ‘blog’ (hawapo pichani), waliohudhuria hafla iliyoandaliwa na kampuni hiyo jana usiku kwenye Hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam. (Picha na Habari Mseto)
 Mtangazaji wa kipindi maarufu cha ‘MiniBuzz’ (zamani Daladala), kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Star TV kwa sasa, Daniel Kijo, ambaye alikuwa mshereheshaji (MC) wa hafla hiyo ya tiGO, akitangaza utaratibu wa kupata washindi wa bahati nasibu ndogo ya washindi wa ‘moderm’ za tiGO. 

 Mwakilishi wa Kampuni ya simu ya tiGO (kulia), akimkabidhi Henry Mdimu zawadi ya ‘moderm’ aliyoshinda katika bahati nasibu ndogo iliyowahusisha wamiliki wa ‘blog’ katika hafla iliyotayarishwa na tiGO. 
 Mtangazaji wa kituo cha televisheni cha EATV, Sam Misago (kushoto), akipokea ‘moderm’ aliyoshinda katika bahati nasibu ndogo kutoka kwa mwakilishi wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo, katika hafla iliyowakutanisha wamiliki na wadau wa magazeti tando ‘blog’ kwenye Hoteli ya New Afrika jana usiku.


Mmiliki wa blog ya Full Shangwe, John Bukuku (kushoto), akipokea zawadi ya  moderm ya tiGO kutoka kwa mwakilishi wa Kampuni hiyo, baada ya kushinda bahati nasibu ndogo katika hafla hiyo.
Wamiliki wa blog, Kambi Mbwana (kulia) na Dina Ismail (katikati), wakiwa katika hafla hiyo ya tiGO.
 Kocha wa kimataifa wa masumbwi, Rajabu Mhamila ‘Super D’ (kulia), akitania kwa kumkunjia ngumi mmilikiwa blog ya Habari Mseto, Fraancis Dande (katikati), huku Mhariri wa Habari Mseto, Salum Mkandemba akishuhudia.

 Mmiliki wa Habari Mseto Blog, Francis Dande (katikati), akiwa na Mhariri wa blog hiyo Salum Mkandemba (kushoto) na Mpiga Picha wake John Dande katika hafla ya tiGO na wadau wa magazeti tando ‘blog’ kwenye Hoteli ya New Afrika jana usiku.  

 Juu: Washiriki wa shindano la kucheza muziki kwa upande wa wanawake, wakionesha umahiri wao katika kucheza muziki wa Twist, kuwania zawadi ya IPad iliyotolewa na tiGO. Chini: Mshindi akikaabidhiwa IPad hiyo na mmoja wa washiriki wa hafla hiyo.


 Mwanamuziki John Mhina wa Tanzanite, akiimba katika hafla hiyo. 
Mshereheshaji ‘MC’aq Daniel Kijo akipozi picha na mmoja wadau walioshiri.
katika hafla hiyo.
ADVERTISEMENT