Picha: Tamasha la chekanao na Vodacom lilivyobamba ndani ya coco beach


Msanii nguli wa muziki wa kizazi kipya Juma Nature akiwapagawisha mashabiki waliofurika katika ufukwe wa Coco beach wakati wa Tamasha la Cheka Nao lilioandaliwa na Vodacom Tanzania kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Wafanyakazi mei mosi juzi jijini Dar es Salaam.


Mwimbaji wa bendi ya muziki wa dansi ya Msondo ngoma baba ya muziki Romarii Mng'anda akiwaongoza waimbaji wenzake wakati wa tamasha la ChekaNao liliandaliwa na Vodacom Tanzania ikiwa ni mahususi kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya wafanyakazi Mei mosi hapo juzi na kufanyika katika ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam.
Wasanii wa Kikundi cha wakali dansi wakionyesha ukali wao wakati wa onyesho la Cheka Nao liliandaliwa na Vodacom Tanzania katika ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam,Ikiwa ni sehemu ya Kusherehekea sikukuu ya Mei mosi hapo juzi .


Msanii anaechipukia wa Kizazi kipya Dogo Lila toka kundi la TMK Wanaume Halisi akionyesha umahiri wake wakati alipokuwa akiimba kwenye Tamasha la Cheka Nao lililoandaliwa na Vodacom Tanzania katika ufukwe wa Coco Beach jijjni Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi Mei mosi hapo juzi.
Previous Post Next Post