Huu ni waraka wa mashtaka wa kesi inayomkabili Lady Jaydee kwenye mahakama ya Kinondoni, Dar es Salaam iliyofunguliwa na Clouds FM.
Jaydee ameandika: Nadhani baada ya hii, maswali yatapungua kama sio kuisha kabisa…Nafahamu kila mtu anasoma kwa wakati wake pengine hamkuona sababu nilizoelezea kwanini sijatoa waraka mwingine Tar 15 kama nilivyo ahidi. Sababu ni kuwa mahakama imesema nisizungumzie hilo swala kwasasa, ambapo kesi bado iko mahakamani…Mpaka nitakapopewa ruhusa ya kuzungumza au kutozungumza tena.”