MTHAILAND AMTWANGA KWA TABU SEGU, BANGKOK




Jonas Segu akipambana vilivyo na Patomsuk Pathompothong kutoka Thailand katika uzito wa Light Welter
























Bondia Jonas Segu chini ya kocha Christopher Mzazi ameonyesha kipaji kikubwa cha kusukuma msumbwi baada ya kupigwa kwa tabu na bingwa wa IBF katika mara la Asia Pacific Patomsuk Pathompothong kutoka Thailand katika uzito wa Light Welter ambaye ni bondia namba 7 duniani katika viwango vya IBF.

Mpambano wao ulifanyika katika jiji lenye mahekalu ya dhahabu la Bangkok na kurushwa na television katika nchi zote za ukanda wa Indo-China za Laos, Myanmar, Cambodia, Vietnam na Thailand yenyewe.

Katika raundi ya 2, 3 na 4 Segu aliuonyesha umati wa mashabiki wa Thailand kuwa yeye kweli ni bingwa mtarajiwa na hakwenda Thailand kula wali wao ila kuiwakilisha nchi yake ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Segu alimhenyesha Pathompothong vilivyo kwa kumchakaza kwa makondde mfululizo hususan akiutumia mkono wake hatari wa kulia ambao ulionekana dhahiri kuwa unaleta madhara makubwa kwa Pathompothong.

Ilididi timu ya wataalam wa Pathompothong kutafakari namna ya kumdhibiti kijana huyo wa Kitanzania ambaye kweli alionekana kuwa alienda Thailand kuuchukua mkanda wa IBF Pan Pacific na sio kufuata ulaji!

Katika raundi ya 6 mabondia wote waliingia ulingoni kama vifaru na kubadilishana masumbwi ya mchanganyiko (combinations) wakitafuta kudhibiti harakati za mpinzani mwenza. Ni katika kubadilishana huku kwa masumbwi ambako Segu aliumizwa mkono na Mthailand Pathompothong.

Kuumia mkono kwa Segu ilikuwa dhahiri kwani mwanzoni mwa raundi ya saba wakati Pathompothong alipokuwa anamiliki ulingo dhidi yake. Segu aliacha pambano hilo katika raundi ya saba wakati mashabiki wengi katika ukumbi huo wakiwa wanaimba Tanzania, Tanzania, Tanzania kwa jinsi alivyokuwa anapeperusha vyema bendera ya “Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”
Previous Post Next Post