CRIS BROWN NA MPENZI KARRUECHE TRAN WAPIGA HATUA,WAHITAJI KUISHI KAMA MKE NA MUME!




Ule usemi wa Kiswahili unaosema ‘penzi ni kikohozi kulificha hauwezi’ unazidi kujidhihirisha kwa Chris Brown pamoja na Karrueche Tran baada ya kuzidi kutoa uhakika wa mapenzi yao yalioingia katika ‘season’ mpya kwa kuanza kuishi pamoja tena.


Chris Brown na Karrueche Tran wamekuwa wakionekana pamoja mara nyingi toka kipindi cha birthday ya Chris (May 5) mwaka huu, na mara zote wameonekana wakiwa katika mazingira ya ‘more than a friend’ kitendo kinachodhihirisha new love chapter kwa couple hiyo ambayo ni miongoni mwa couple za mastaa zinazostahili ‘tuzo ya drama’ kama zingekuwepo!

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ Chris na Karrueche wamekuwa wakiishi pamoja toka warudiane na tayari Karrueche ameshahamishia baadhi ya nguo zake na vitu binafsi vidogo vidogo. Hata hivyo katika hali ya tahadhari Karrueche hakuhamisha vitu vyake vyote, ili endapo episode za furaha zikifikia ukingoni asipate shida kurudi kwake!
Previous Post Next Post