WAZIRI GHASIA ATAKA USIMAMIZI MAKINI KATIKA MASUALA YA MANUNUZI

WAZIRI wan chi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, ( TAMISEMI) Hawa Ghasia, amezitaka Kamati za Fedha na Uongozi za Halmashauri za Wilaya, Miji na Majiji nchini kuhakikisha wanasimamia masuala ya manunuzi kwa uadilifu na ufanisi mkubwa ili kuhakikisha kuwa fedha za umma zinawanufaisha walengwa. 
 Pia amezitaka Kamati hizo kuepuka kashfa zisizokuwa na sababu wakati wa manunuzi unapofanyika katika Halmashauri zao na kutaka wazingatie sheria , kanuni na utaratibu mzima katika hatua zote za suala hilo. Waziri Ghasia alisema hayo katika hotuba yake ya ufunguzi mafunzo yaliyohusu mambo muhimu ya kuzingatia katika ununuzi kwa Wenyeviti wa Kamati za Fedha na Uongozi wa Halmashauri zote za Tanzania Bara. 
Wenyeviti hao na viongozi wa Kamati hizo walishiriki mafunzo hayo ya siku tatu yaliyoanza Aprili 22 na kufukia tamati Aprili 24, mwaka huu mjini Morogoro ambayo yaliandaliwa na Uongozi wa Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Ununuzi wa Umma ( PPRA). 
 Alisema , lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha fedha zinazotumika ziweze kuleta manufaa zaidi kwa walengwa ambao ni wananchi ambao wanatarajia kupata huduma zilizo bora na kwa gharama nafuu. Waziri Ghasia alisema ,asilimia zaidi ya 70 ya bajeti ya kawaida na asilimia 100 ya bajeti ya maendeleo imekuwaikitumika katika kufanya manunuzi. 
 Kwa mujibu wa Waziri hiyo, takiwmu nyingine zinaonesha kuwa ununuzi unaweza kugharimu takriban asilimia 15 hadi 20 ya pato la taifa (GDP). 
 “ Hali hii, inaonesha ni jinsi gani Serikali yetu inavyotumia fedha nyingi katika sekta hii muhimu kwa ajili ya kuleta maendeleo yanayolenga ufanisi wa kiutendaji “alisema Waziri Ghasia na kuongeza. 
 “ Jambo hili litaleta tija katika uwajibikaji na kuleta hali bora ya maisha kwa raia wote tunaowatumikia” alisisitiza Waziri huyo. 
 Alisema , Serikali inatambua umuhimu wa Kamati hizo katika kutekeleza majukumu yaliyoainishwa kwa mujibu wa sheria , kanuni na taratibu zilizowekwa. Waziri Ghasia alisema, mafunzi hayo na maboresho ya mfumio wa ununuzi lengo kuu ni kupata thamani inayilingana na ubora pale fedha za umma zinapotumika kununu bidhaa , huduma au kandarasi za ujenzi. 
 “ Utafiti unaonesha kuwa endapo hizi Kamatyi zitapata mafunzo ya sheria ya Ununuzi kutaongeza ufanisi na tija katika uendeshaji wa Halmashauri zetu” alisema Waziri Ghasia. 
 Hivyo aliwataka Viongozi wa Kamati hizo kuhakikisha kuwa mafunzo waliyopata mara akirejea katika Halmashauri zao waashirikishe Madiwani ambao hawakupata nafasi ya kuhudhuria mafunzo hayo ili watambue wajibu wao wa kusimamia fedha za umma.
 Waziri wa Tamisemi, Mhe Hawa Ghasia akikaribishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya PPRA, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo ( kushoto) akimwongoza Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia baada ya kufungua mafunzo. Wa pili kulia ni Nkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe Joel Bendera.
 Waziri wa Tamisemi,  Mhe Hawa Ghasia akiwahutubia wenyeviti na viongozi wa kamati za fedha na uongozi za Halmashauri za Wilaya nchini

Waziri wa Tamisemi, Mhe Hawa Ghasia ( mwenye ushungi ) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Morogoro na wenyekiti na viongozi wa Kamati za fedha na uongozi za Halmashauri zote nchini
Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA