WAKULIMA WA MIWA WAISHITAKI SERIKALI KWA CCM,CCM YAPANGA KUONANA NAO JUMATATU MJINI MOROGORO.


Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Wakulima wa Miwa sambamba na Uongozi wa Kiwanda cha Sukari Mtibwa,kwenye mkutano wao uliofanyika kwenye ukumbi wa hotel ya Honolulu,Turiani wilayani Mvomero,Morogoro.Mkutano huo umefanyika huku ukiwashirikisha wakulima,uongozi wa Kiwanda na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero,kufuatia Wananchi wa Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro kukishitaki Kiwanda cha Sukari Mtibwa kuwa kimekuwa kikifanya dhuluma kubwa dhidi ya wakulima wa miwa huku wakimuomba Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), kufanya kila analoweza kuhakikisha mgogoro uliopo kati ya pande hizo mbili unapatiwa ufumbuzi. Aidha chama cha CCM kimetoa maelekezo ya kukukutana na Wakulima hao pamoja na uongozi wa Kiwanda cha Mtibwa siku ya jumatatu,kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo.




Baadhi ya Wakulima wa Kiwanda cha sukari Mtibwa na Uongozi wa Kiwanda hicho wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wao na Uongozi wa juu wa CCM,mapema leo uliofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Honolulu,Turiani Wilayani Mvomero .


Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza mbele ya wakulima wa miwa na uongozi wa Kiwanda cha sukari Mtibwa kuhusiana na Mgogoro wao mkubwa uliodumu takribani kwa miaka 10 sasa,aidha Uongozi wa CCM umesikiliza pande zote mbili (Wakulima wa miwa & Uongozi wa Kiwanda cha Mtibwa) na kuamua kukukutana na Wakulima hao pamoja na uongozi wa Kiwanda cha Mtibwa siku ya jumatatu,kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo.


Mmoja wa Wakulima wa Miwa kutoka kiwanda cha sukari Mtibwa,Mzee Pascal akizungumzia tuhuma na dhuluma mbalimbali wanazofanyiwa na uongozi wa Kiwanda hicho,Aidha Mzee Pascal alisema kuwa wakulima wa miwa wamekuwa na mgogoro na kiwanda hicho uliodumu kwa miaka 10 sasa,lakini kwa bahati mbaya hakuna majibu ya suluhu hali inayofanya wananchi wajiulize maswali bila majibu. Mzee Pascal aliyataja baadhi ya matatizo makubwa yanayofanywa na kiwanda cha Mtibwa kuwa ni kucheleweshwa kwa malipo ya miwa, kiwango kidogo cha malipo pindi wanapopeleka mazao yao kuuza kiwandani, madeni sugu kwa wastaafu wa kiwanda lakini kubwa zaidi wanadai kuna dhuluma ambayo imekuwa ikifanywa na uongozi wa kiwanda hicho.


Mmoja wa Wastaafu wa Kiwanda cha sukari Mtibwa,akikishitaki kiwanda hicho mbele ya Uongozi Mkuu wa CCM,kuhusiana na malimbikizo ya mafao ya PPF,ambayo yamekuwa yakileta mgogoro mkubwa kati yao kutokana na kutolipwa kwa wastaafu hao.



Mwenyekiti wa halmashauri Wilaya ya Mvomero ,Bwa.Jonas Van Zeiland akizungumza mbele ya Uongozi wa CCM,chini ya uongozi wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana uliofika Turiani,Wilayani Mvomero uliofika kusikiliza na kutafuta ufumbuzi wa Changamoto/Mgogoro uliopo kati ya Mwekezaji wa Kiwanda cha Sukari Mtibwa na wakulima wa Miwa.


Meneja wa kanda ya Mvomero-PPF,Bwa.John Mwalisu akitoa ufafanuzi mbele ya wakulima wa Miwa-Mtibwa,kuhusiana na malimbikizo yao ya mafao ya Kustaafu kutoka kwa Mwekezaji wa kiwanda cha sukari cha Mtibwa, kwamba Kiwanda hicho kimekuwa kikishindwa kuwalipa wastaafu mafao yao na hata wakienda mahakamani wanashangaa wanashindwa kesi na mwekezaji kuibuka mshindi hata katika kesi zao za msingi za madai.


Mratibu kutoka Uongozi wa Kiwanda cha Sukari Mtibwa,Bwa.Hamad yahaya akijibu tuhuma na dhuluma mbalimbali zilizoelekezwa kwa mwekezaji wa Kiwanda hicho pamoja na uongozi mzima kutoka kwa Wakulima wa MiwaKufuatia tuhuma hizo wakulima wa miwa na wawakilishi wao walimwambia Kinana aliyeambatana na viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama cha CCM akiwemo Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, walisema mgogoro umedumu kwa miaka 10 lakini kwa bahati mbaya hakuna majibu ya suluhu hali inayofanya wananchi wajiulize maswali bila majibu.Aidha uongozi wa Kiwanda cha Sukari Mtibwa umeweka wazi kuwa kinatambua baadhi ya changamoto zilizopo baina yao na wakulima na kwamba sasa ni wakati wa kutafuta ufumbuzi wake na kuanza ukurasa mpya lakini pia wakaomba CCM kuiomba Serikali kuangalia wawekezaji wa ndani kwani kuna sukari inayotoka nje na kufanya wakose fedha.


Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa,Nassor Seif mara baada ya mkutano na Wakulima wa Miwa,Uongozi wa Kiwanda hicho pamoja na Uongozi wa juu wa CCM kukutana kwa pamoja na kusikiliza matatizo yaliyomo,uliofanyika mapema leo mchana kwenye ukumbi wa hotel ya Honolulu,Tuliani wilayani Mvomero,Morogoro.Mkutano huo umefanyika kufuatia Wananchi wa Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro kukishitaki Kiwanda cha Sukari Mtibwa kuwa kimekuwa kikifanya dhuluma kubwa zidi ya wakulima wa miwa huku wakimuomba Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), kufanya kila analoweza kuhakikisha mgogoro uliopo kati ya pande hizo mbili unapatiwa ufumbuzi.
Previous Post Next Post