Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Miliki ya Rasilimali za Reli(RAHCO), Mhandisi Benhadard Tito(aliyevaa miwani) akitoa maelezo ya namna RAHCO ilivyojipanga kuboresha njia za reli katika eneo lilioathirika na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wa Wizara ya Uchukuzi leo mchana walipotembelea eneo hilo kujionea namna mvua zilivyoathiri Njia za Reli ya USafiri wa Treni Dar es Salaam.
Eneo lililoharibiwa na mvua zilizonyesha hivi karibuni na kuondoa kingo zilizo karibu na Reli katika eneo ya tabata Mwananchi. Wajumbe wa baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Uchukuzi wametembelea eneo hilo kuona uharibifu uliofanywa na Mvua hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania(TRL), Mhandisi Aman Kisamfu akitoa maelezo ya namna mvua zilivyoletaa uharibu katika eneo la tabata Mwananchi kwa Wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Uchukuzi leo mchana.Wajumbe wa Baraza hilo walitembelea eneo hilo na kuona uharibifu mkuwa uliofanywa na mvua zilizonyesha hivi karibuni.Kulia kwa Mkurugenzi Mkuu wa TRL ni Katibu Mkuu wa Wizara ya
Uchukuzi,Mhandisi Omar Chambo(Mwenye Shati jeupe).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo, akitoa maelekezo kwa Mkurgenzi Mkuu wa Shirika la reli Tanzania(TRL) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Miliki ya Rasilimali za Reli(RAHCO), wakati wa Ziara iliyofanywa na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Uchukuzi katika eneo la Reli lililoharibiwa na mvua leo mchana.