VODACOM YAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA KATIKA SHULE ZA MSINGI VIJIJINI

* Yakamilisha ukarabati wa vyumba vya madarasa Chunya 
* Kunufaisha zaidi ya wanafunzi 200 

Uchakavu wa miundombinu ya shule hasa za msingi nchini ikiwemo vyumba vya madarasa ni moja ya chanzo kikuu kinachodhoofisha mahudhurio ya wanafunzi na hivyo kusababisha matokeo yasiyoridhsiha Aidha katika kusaidia taifa kukabiliana na changamoto hiyo kampuni ya Vodacom Tanzania kupitia Mfuko wake wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation imeendelea kutoa mchango kwa jamii kwa kuhakikisha shule zinakuwa na miundombinu yenye kuhusiha wanafunzi kufundishika na pia kupenda shule. 

Mwishoni mwa wiki Vodacom Foundation ilikabidhi vyumba vitatu vya darasa katika shule ya Msingi Mkwajuni iliyopo katika kijiji cha Mkwajuni Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya baada ya kuvifanyia marekebisho makubwa ambavyo yanatazamiwa kupunguza tatizo la utoro shuleni hapo. Aidha imekabidhi pia na madawati 30 Vyumba Hivyo vitatumika kwa ajili ya wanafunzi zaidi ya 200 wa darasa la nne na la tano shuleni hapo . 
"Tumekuwa na changamoto kubwa ya wanafunzi kutopenda kuja shuleni na hii inasababishwa na shule kuwa na miundombinu chakavu isiyowapa ari ya kusoma wanafunzi na pia kukosekana wka huduma ya chakula cha machana hapa shuleni."Alisema Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule hiyo Florence Simsokwe wakati akipokea vyumba hivyo vya madarasa mwishoni mwa wiki. 
Aidha Mwalimu Simsokwe ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa wanakijiji cha Mkwajuni kuona thamani ya vyumba Hivyo ambavyo kwa sasa vipo katika mwonekano na njia pekekee ya kufanya Hivyo ni kulinda mwonekano huo kama sehemu ya kuonesha shukrana na kuwapa moyo wahisani zaidi kujitokeza kuendelea kuiboresha shuel hiyo.
 "Tangu madarasa haya yalipoanza kukarabatiwa wanafunzi wamekuwa na shauku kubwa kuanza kuyatumia na hili limekuwa faraja kwetu Hivyo ni wazi kwamba yatatusaidia kuongeza kiwango cha mahudhurio shuleni na hatiame kuongeza ufaulu."Aliongeza Mwalimu Simsokwe.
 Akipokea vyumba Hivyo kutoka Vodacom Foundation na baadae kuvikabidhi kwa uongozi wa shule kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Sosthenes Mayoka amesema kukabidhiwa kwa madarasa hayo ni hatua moja ila hatua muhimu ni kuhakikisha matunzo yake ili yatoe tija. "Mdarasa mazuri ya aina hii huvutia mahudhurio Hivyo ni lazima wazazi wawe tayari kusaidia hatua za haraka kufanyia amtengenezo mara tu tatizo linapojitokeza na kabla halijawa kubwa na kugharimu kiasi kikubwa cha fedha. Kwa njia hiyo madarasa haya yatadumu." Alisema Mayoka 
Amesema juhudi zinazooneshwa na Vodacom katika kusaidia jamii zinaendana na imani ya serikali kwamba changamoto katika sekta ya Elimu nchini zinahitaji Nguvu ya Pamoja kati ya serikali, wahisani, walimu na wazazi.
 Kwa upande wake Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule amesema kazi iliyofanywa shuleni hapo na mfuko huo ni sehemu ya utekelezaji wa azma ya Vodacom kusaidia kuboresha amzingira ya shule kwa lengo la kuhuisha watoto kusoma vizri na hatiame kufaulu.
 "Leo tunakabidhi vyumba vya madarasa hapa Mkwajuni Shule ya Msingi ila kazi hii imekuwa ikifanyika nchi nzima kwa kujenga vyumba vipya vya madarasa, kukarabati na kuwezesha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano shuleni.
 "Tunajiskia furaha kuwekeza katika jamii kwa kiwango ambacho kinaleta tofauti kubwa sana kati yetu na makampuni mengine ya biashara hapa nchini. Leo nanyi mnakuwa mashuhuda wa utofauti wetu na wengine, Vodacom sio tu inaongoza soko katika utoaji wa huduma bora bali pia namna tunavyojali wanaotuzunguka"Aliongeza Mwakifulefule.
 Vodacom Foundation imetumia kiasi cha Sh 500 Milioni kusaidia sekta ya elimu nchini katika kipindi cha mwaka 2012/ 2013 ikiwemo msaada huo wa Mkwajuni Shule ya Msingi.
 Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim (katikati) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule (kulia) na Katibu wa Mbunge wa Songwe Agapito Kilongozi kabla ya kuanza kwa hafla ya makabidhiano ya vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi Mkwajuni Wilayani Chunya mwishoni mwa wiki.
 Katibu Tawala Wilaya ya Chunya Sosthenes Mayoka akikabidhi funguo za vyumba vitatu vya madarasa kwa Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Mkwajuni Wilayani Chunya baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa na Vodacom Foundation. Anaeshuhudia ni Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule. Hafla hiyo imefanyika mwishoni mwa wiki.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mkwajuni Wilayani Chunya Mkoa wa Mbeya wakifuatilia kwa furaha hafla ya makabidhiano ya vyumba vitatu vya madarasa vilivyofanyiwa ukarabati mkubwa na Vodacom Foundation katika mikakati yake ya kuchangia maendeleo ya sekta ya elimu nchini. Hafla hiyo ilifanyika shuleni hapo mwishoni mwa wiki iliyoongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Chunya Sosthenes Mayoka.
 Wanafunzi wakifurahia madarasa mapya
Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim akiwa na wanafunzi wa darasa la sita wa shule ya msingi Mkwajuni Wilayani Chunya Jackson Anthon (kulia) na mwenzake Erica Agustino. Wanafunzi hao walijibu kwa ufasaha maswali ya ufahamu wa huduma za Vodacom ya Cheka nao na M-pesa wakati wa hafla ya makabidhinao ya vyumba vitatu vya madarasa vilivyokarabitiwa na Vodacom Foundation. Vodacom Foundation imeahidi kuwapatia wanafunzi hao vifaa vya shule, sare na vitabu vya kiada kwa ajili ya darasa la sita na la saba.
Previous Post Next Post