Peter Ngota Afisa Mkuu wa Mauzo na Masoko akionyesha moja ya simu zinazouzwa na kampuni hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika jengo la makao makuu ya kampuni ya TTCL mtaa wa Samora wakati kampuni hiyo ilipozindua rasmi huduma za Bando na TTCL na Basti leo jijini Dar es salaam kulia ni Kisamba Tambwe Mkuu wa Mauzo Kampuni ya TTCL.
Peter Ngota Afisa Mkuu wa Mauzo na Masoko akionyesha kampeni ya Bando na TTCL mara baada ya kuizindua rasmi kushoto anayepiga makofi ni Ernesti Isaya Mkuu wa Maendeleo ya Bidhaa TTCL. Peter Ngota Afisa Mkuu wa Mauzo na Masoko akionyesha kampeni ya BASTI ambayo ina viwango vipya vya muda wa kuperuzi kwenye mtandao wa kampuni hiyo.
…………………………………………………………………………
TTCL, imezindua huduma mpya ya Bando Na TTCL inayoambatana na punguzo
kubwa la bei kwa huduma ya INTERNET. Mtakumbuka ni Juzi tu tareha 21 Machi 2013
tulifungua kituo chetu kipya cha huduma kwa wateja kilichopo Kariakoo katika mkoa
wa Dar es Salaam katika kupanua mtandao wa huduma kwa wateja nchini (>30 CSC
network nchini).
Kifuatacho sasa ni kupanua wigo wa huduma kwa wateja.
Vilevile mtakumbuka kuwa baada ya kujitambulisha sokoni na huduma ya ‘Mobile Internet’
isiyo na kikomo ya BANJUKA; kampuni ya simu ya TTCL sasa inazindua huduma mpya
inayojulikana kama ‘BANDO NA TTCL’. Huduma hii inamuwezesha mteja kufaidika na meseji
za bila kikomo, kuperuzi intaneti na muda wa maongezi kwenda mitandao yote kwa wakati
mmoja kwa bei hadi ya shilingi 500. BANDO NA TTCL inawalenga zaidi watumiaji wa simu za
kisasa za smart phones za TTCL (zinazopatikana ktk vituo vya huduma kwa wateja
nchini). Maelezo zaidi ya juu ya huduma hii yanapatikana kwa kupiga 100 huduma kwa wateja
au tembelea ofisi zetu za mauzo zilizoenea nchi nzima.
Aidha, TTCL imeshusha kwa kiwango kikubwa bei ya vifurushi vyake vya mobile internet kwa
kampeni ya BASTI ikimaanisha peruzi intaneti zaidi kwa gharama nafuu. Hili ni punguzo la bei
la aina yake. Mathalani; kifurushi cha mwezi cha 4GB kilichokuwa kinauzwa shilingi 90,000
sasa kinauzwa kwa shilingi 25,000 tu. Hii ni nafasi si tu kwa wateja waliopo wa TTCL kuongeza
matumizi kwa gharama nafuu bali hata kwa wateja wapya ikiwamo watumiaji wadogo kujiunga
na mtandao wa TTCL. (Haki ya mawasiliano kwa wote)
Leo hii, wateja wengi zaidi na hasa wanafunzi na wajasiliamali wanatumia simu za kisasa (smart
phones, tablet PCs kama iPad, Samsung Galaxy nk) na kompyuta ili kupata huduma za intaneti
na mitandao ya kijamii kwa mfano, Michuzi blog, facebook twitter, LinkedIn n.k ) kwa shughuli
zao za kila siku. Upatikanaji wa vifaa hivi vya kisasa (sambamba na ukuaji wa teknolojia) na
kumewezesha kukua kwa kasi kwa tabaka la kati lawatumiaji hivyo kumesababisha kukua
maradufu kwa soko la intaneti hapa nchini. (Hili nijambo jema sana kwa nchi yetu na maendeleo
ya watu wake kiuchumi na kijamii)
Kwa kuzingatia haya (na kutambua kuwa mawasiliano na habari ni swala mtambuka), TTCL ina
mikakati wa kuwawezesha wananchi wengi zaidi kupata huduma za intaneti na mawasiliano &
habari kwa ujumla na hivyo kuwa chachu kubwa ya maendeleo nchini. Huduma mpya ya
BANDO NA TTCL na kampeni ya BASTI ni juhudi za makusudi za TTCL katika kutimiza
adhma hii.