Mkuu wa wilaya ya Lindi Dr Nasor Ally Hamid akisoma hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi katika Uzinduzi wa wiki ya Chanjo ambapo Mkoa wa Lindi kwa Mwaka 2012 imeshika nafasi ya Kwanza Kitaifa..Maadhimisho hayo kimkoa yamefanyika katika kata ya Mingoyo shule ya msingi Mnazi mmoja Lindi.
Mtoto Fatma Issa akipewa chanjo na Mkuu wa Wilaya ya Lindi katika Uzinduzi wa WIKI YA CHANJO.
Kaimu Mganga mkuu wa mkoa wa Lindi,Dr Sonda Yusuf akitoa taarifa ya chanjo na changamoto zake katika Maadhimisho hayo.
Mratibu wa chanjo mkoa wa Lindi Bi Zainab Mathradas akitoa taarifa za chanjo mkoa wa Lindi huku akitoa wito kwa akina Baba kwenda kliniki sambamba na akina mama ili wapatiwe vipimo na chanjo mbalimbali.
Wadau wakisiliza hotuba ya uzinduzi wa wiki ya chanjo.
MAADHIMISHO ya Wiki ya Chanjo kitaifa Mkoa wa Lindi yamezinduliwa leo huku Mkoa huo ukishika nafasi ya kwanza Kitaifa kwa kuvuka lengo la kutoa chanjo mwaka 2012.
Maadhimisho hayo yalizindiliwa jana kitaifa mkoani Pwani na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete yatatumika katika kuhamasisha na kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa chanjo pamoja na kuwasisitiza wazazi kuwapeleka watoto kwenye vituo vya afya ili kupata huduma ya chanjo.
Akizindua Maadhimisho hayo kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Mkuu wa wilaya ya Lindi,Dr Nasor Ally Hamid alieleza kuwa Mpango utakaosaidia kutokomeza magonjwa kama vile kifua kikuu, kifaduro, polio, nimonia, pepopunda, homa ya ini na uti wa mgongo pamoja na kuzuia vifo vya watoto.
Pamoja na kushika nafasi ya kwanza Kitaifa kwa kiasi kikubwacha kuwapatia chanjo watoto walio na umri wa chini ya mwaka mmoja kwa zaidi ya asilimia 80 ambao wako katika hatari ya kupata maambukizi ya magonjwa hayo Wito umetolewa Kwa Akina Mama kujitokeza kupata chanjo hizo kufuatia kubainika kuwa watoto hawajapata chanjo na wengine kutokamilisha chanjo hizo.
Akiongelea Maadhimisho hayo yenye kauli mbiu ‘Okoa maisha, jikinge na ulemavu Pata chanjo.’Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Dr Sonda Yusuf Shaban alizitaka Halmashauri kuongeza ununuzi wa gesi na majokofu ili kusaidia uzuiaji wa magonjwa kupitia chanjo mbalimbali Sambamba na Uzinduzi huo.
Mratibu wa Chanjo Mkoa,Bi Zainab Mathradas alitoa wito kwa akina mama kuacha kuzalia Nyumbani ikiwa pamoja na akina baba kuhudhuria Kliniki kwa Vipimo mbalimbali ambavyo vimeanza kutolewa sambamba na akina mama wajawazito.
Mkoa wa Lindi una jumla vituo 238 vya huduma ambapo kati ya hivyo ni 197 tu vinavyotoa huduma za chanjo kiwango cha utoaji huduma hiyo ikiongezeka kwa asilimia 7 na kuvuka lengo la kitaifa kwa asilimia 98 badala ya 80 iliyopangwa