Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitia saini katika kitabu cha maombolezo wakati alipofika mkoani Arusha jana Kuwapa pole ndugu na jamaa ambao nduguzao wamefariki katika machimbo ya Moramu katika eneo la Moshono Mkoani Arusha maporomoko hayo yametokea juzi nakusababisha vifo vya watu kumi na tatu na majeruhi wawili ambao mmoja ameruhusiwa na mwingine amelazwa katika Hospitali ya Maunti meru
Majeneza ya watu waliofariki katika ajali hiyo yakiwa yamepangwa tayari kwa mazishi
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa katika msiba huo na viongozi wa mkoa wa Arusha
Mmoja wa viongozi wa dini ya kiislamu akiombea miili hiyo ya marehemu tayari kwa ajili ya kuzikwa
Waziri Mkuu Mizengo pinda akiwapa pole ndugu jamaa na marafiki waliopoteza ndugu zao katika ajali hiyo ya kufukiwa kwa wachimbaji wa madini ya moramu huko Moshono mkoani Arusha