LOWASSA KUKABIDHIWA TUZO YA HESHIMA IRINGA JUMAPILI

dala
MH.EDWARD LOWASSA



ask
Askofu Dkt Boaz Solla akiwa na waumini wake

WAUMINI na uongozi wa huduma ya injili na uponyaji ya Overcomers Power Center (OPC) chini ya Askofu Dkt Boaz Sollo inategemea kumtunuku tuzo ya heshima kwa mchango wake mkubwa katika Taifa waziri mkuu mstaafu wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Edward Lowassa katika hafla maalum itakayofanyika siku ya jumapili mjini Iringa .

Waumini hao wameandaa maandamano makubwa ya amani kwa ajili ya kumpokea Lowassa kutoka katika uwanja wa Ndege Nduli majira ya saa 3 asubuhi atakapowasili kwa Ndege na kuelekea katika ukumbi wa St Dominic ambako kutafanyika shughuli hiyo kuanzia muda wa saa 6 mchana .

Akizungumza na waandishi wetu askofu Dkt Sollo alisema kuwa mbali ya kumtunuku tuzo hiyo Bw Lowassa pia kiongozi huyo anataongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa jengo la kanisa la OPC linaloendelea kujengwa katika eneo la zizi la Ng’ombe ambapo zaidi ya Tsh. Milioni 250 zinahitajiika kukamilisha ujenzi wa jengo hilo pamoja na kituo cha Radio Overcomers Fm (98.6 Mhz)kilichopo mjini Iringa .

Dkt Sollo alisema kuwa lengo la OPC kumwalika na kumtunuku tuzo ya heshima Bw Lowassa ni kutokana na kuwa jirani zaidi na jamii na amekuwa akiitika wito wa makundi mbali mbali na kuyasaidia bila ubaguzi wowote hivyo kutokana na mchango wake huo kwa jamii wao kama kanisa wameona ni vema kuutambua mchango wake huo na kumwalika ili kumpa tuzo hiyo maalum kama ahsante kwake.

“ Tuzo hiyo itampa moyo zaidi wa kuendelea kuwa karibu na jamii na kutambua pia mapokeo ya jamii ambayo amekuwa akiisaidia mara kwa mara ….ikiwa ni pamoja na kuendelea kusaidia kuendeleza amani nchini kwa kuchangia nyumba za ibada”

Pia alimtaka Lowassa kuendelea kusaidia jamii bila kuchoka hata kama baadhi ya watu wasiopenda jitihada zake kuendelea kutoa maneno yenye kumkatisha tamaa na kuwa siku zote kile anachokifanya jamii inakitambua na Mungu ndie ajuaye na ndie mtoa baraka kwake.

Dkt Sollo alisema kuwa Lowassa ambae ni mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha amekuwa kipenzi cha wengi hata wale wasio wapiga kura wake na kuwa uongozi wake kama waziri mkuu wengi walitokea kumpenda na kuwa toka alipojiuzulu nafasi hiyo ya uwaziri mkuu hajapata kufika mkoani Iringa hivyo sehemu kubwa ya wana Iringa wana hamu kubwa ya kukutana nae kwa mara nyingine.

Hata hivyo baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Iringa wamepongeza hatua ya OPC chini ya Dkt Sollo kuamua kumtunuku tuzo hiyo Lowassa na kuwa ni kweli anastahili kupewa tuzo kwani ni miongoni mwa viongozi waadilifu na wachapa kazi hapa nchini.

Anania Sanga alisema kuwa kuna kila sababu ya viongozi kama Lowassa kuendelea kuthiaminiwa kama ambavyo OPC ilivyoamua kuutambua mchango wake kwa kukusudia kumtunuku tuzo hiyo maalum ambayo si heshima kwa kituo hicho cha OPC pekee bali ni heshima ya mkoa wa Iringa ni mfano kwa viongozi wengine kufanya kazi ya jamii kwa ufanisi zaidi ili kuja kupongezwa na jamii kama hivyo .
Previous Post Next Post