KINANA NA NAPE WAITEKA MOROGORO KATIKA MKUTANO WA KUHITIMISHA ZIARA YAO MKOANI HUMO LEO

Kinana akihutubia Wananchi

katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia umati wa wananchi katika Uwanja wa Uwanja wa Ndege (zamani sabasaba) mjini Morogoro leo, Aprili 21, 2013, ikiwa ni hitimisho la ziara yake ya siku nane aliyofanya katika wilaya zote, mkoani Morogoro.



Baadhi ya maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa CCM kwenye Uwanja wa Kiwanja cha Ndege wa mjini Morogoro, wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipokuwa akizunguma Uwanjani hapo.


Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na uenezi Nape Nnauye akizungumza katika mkutano huo uliwakutaanisha wakazi mbalimbali wa mji wa Morogoro mapema leo jioni wakati chama hicho cha CCM,kilipokuwa kikihitimisha ziara yake ya siku nane mkoani humo.





Msanii wa muziki wa kizazi kipya ajulikanae kw jina la Abdul Nasib a.k.a Diamond akitumbuiza jukwaani jioni ya leo kwenye hitimisho la mkutano wa chama cha CCM,uliofanyika kwenye uwanja wa Ndege (zamani Sabasaba),Mkoani Morogoro.Uongozi wa Chama hicho ukiongozwa na Katibu Mkuu wake,Ndugu Abdulrahman Kinana wamefanya ziara ya kutembelea wilaya zote saba za mkoa huo kukagua uhai wa chama na maendeleo ya miradi mbalimbali.


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, nape Nnauye wakiingia katika Uwanja wa Mkutano wa hadhara wa Kiwanja cha Ndege, mjini Morogoro, leo

Baadhi ya maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa CCM kwenye Uwanja wa Kiwanja cha Ndege wa mjini Morogoro, wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipowasili Uwanjani hapo.




Umati ukiwa umefurika kwenye mkutano wa CCM uliofanyika leo April 21, 2013 kwenye uwanja wa Kiwanja cha Ndege wa mjini Morogoro.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa kata ya Kichangani,Bi.Fatma Said,mara baada ya kuzindua mradi huo kwenye kata hiyo,wilaya ya Morogoro mjini mapema leo mchana.Aidha Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini,Mh Mohammed Aziz Abood alisema kuwa hiyo ni sehemu ya mradi wa visima 23 vilivyochimbwa kwenye Manispaa ya mji huo na kwamba visima hivyo vya maji vimegharimu kiasi cha shilingi Milioni 365.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipewa zawadi ya dumu la sabuni ya maji,inayotengenezwa na kikundi cha akina mama wajasiliamali kiitwacho Chemchem kilichopo mtaa wa Mfungua Kinywa ndani ya kata ya Mwembesongo.Kikundi hicho kimejikita zaidi kwenye ujasiliamali wa kutengeza sabuni,Mradi wa kuweka na kukopa,biashara za mboga mboga.Ndugu Kinana alikichangia kikundi hicho kiasi cha zaidi ya shilinnigi milioni mbili.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipandisha bendera mara baada ya kulizindua shina la kikundi cha akina mama wajasiliamali kiitwacho Chemchem kilichopo mtaa wa Mfungua Kinywa ndani ya kata ya Mwembesongo.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikata utepe ndani ya kata ya kichangani kuashiria uzinduzi wa Visima vya maji vipavyo 23 vilivyopo ndani ya Manispaa ya Morogoro mjini,vilivyojengwa na Mbunge wa jimbo hilo Mh Mohammed Aziz Abood wa pili kulia .

Maji yanatoka safi kabisa kwa ajili ya kuwahudumia wanakijiji wa kata ya Kilongo.



Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na baadhi ya wakazi wa kata ya Kilongo,mara baada ya kuzindua mradi wa maji,kwenye wilaya ya Morogoro mjini mapema leo mchana.Aidha Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini,Mh Mohammed Aziz Abood alisema kuwa hiyo ni sehemu ya mradi wa visima 23 vilivyochimbwa kwenye Manispaa ya mji huo na kwamba visima hivyo vya maji vimegharimu kiasi cha shilingi Milioni 365.

Previous Post Next Post

Popular Items