Katika suala la ajira, Uhuru alieleza kwamba upo umuhimu wa kuwawezesha vijana na wanawake kupata ajira, mfuko maalumu umeanzishwa, ambapo fedha za miradi zitatakiwa kupelekwa kwenye ngazi ya majimbo. wa huduma za jamii, kuzalisha nafasi za ajira, elimu, ulinzi, kuboresha miundombinu na kuwa na Serikali itakayosaidia kuimarisha umoja wa kitaifa.
“Serikali yangu pia itasimamia sheria ipasavyo ikiwamo kuwasilisha miswada bungeni na kusimamia utekelezaji wa Katiba Mpya ya nchi hiyo.
“Pia suala la usalama ni muhimu sana, tunatakiwa kuongeza idadi ya polisi, kuwajengea uwezo wa vifaa na kuboresha masilahi yao,” alisema Kenyatta.
Katika suala la elimu, Kenyatta alisema wanafunzi wote watakaoanza darasa la kwanza mwaka kesho na wale wanaoingia vyuo vya elimu ya juu watapatiwa kompyuta pakatwa (laptop).
Hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi zake alizotoa wakati wa kampeni iliyompa ushindi.
Alieleza kwamba vyuo vya elimu ya juu pia vinatakiwa viongezwe kwenye kaunti zote ili kuzuia vyuo vya elimu ya kati kutumika kama vyuo vikuu.
Katika suala la ajira, Uhuru alieleza kwamba upo umuhimu wa kuwawezesha vijana na wanawake kupata ajira, mfuko maalumu umeanzishwa, ambapo fedha za miradi zitatakiwa kupelekwa kwenye ngazi ya majimbo.
Kenyatta alisema kwamba kwa sasa upo umuhimu wa kuangalia zaidi kwenye mapinduzi ya viwanda na kuhakikisha kwamba wanaandaa na kuboresha bidhaa za ndani.