JAPAN YATOA BILIONI 129.4 KUIMARISHA SEKTA YA BARABARA

Waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa wa kwanza kushoto akisaini mkataba wa makubaliano ya mkopo wenye riba nafuu kwajili ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami, kulia ni Balozi wa Japani nchini Tanzania Bwana. Masaki Okada akitia saini pia makubaliano hayo.

Waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa akibadilishana hati za makubaliano ya mkataba na Balozi wa Japani nchini Tanzania Bwana. Masaki Okada, mkataba huo utaiwezesha Tanzania kukamilisha awamu ya pili ya ujenzi wa barabara hizo kwa kiwango cha lami.Waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa akisisitiza jambo akiwa na Balozi wa Japani nchini Tanzania Bwana. Masaki Okada mara baada ya kukamilisha kwa shughuli za utiliaji saini wa makubaliaono ya mkopo wa riba nafuu.


Serikali ya Tanzania imetiliana saini mkataba na JAPAN wa shilingi Bilioni 129.4 ambao mkopo wa masharti nafuu kupitia shirika lake la maendeleo JICA kwa ajili ya kuendeleza sekta ya barabara nchini.

Fedha hizo ni kwa ajili ya kutekeleza mradi wa barabara awamu ya pili kwa kiwango cha lami itahusisha urefu wa kilomita 203 ambayo ni kutoka Mtambaswala, Mangaka hadi Tunduru kwenye ukanda wa Mtwara barabara hii ambayo inaunganisha kusini mwa Tanzania pamoja na Msumbiji, Malawi na Zambia.

Sherehe hizo za utiaji wa saini zimefanyika leo jijini Dar es salaam ambapo Tanzania iliwakilishwa na Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa na Japan iliwakilishwa na Balozi Masaki Okada.

Kwa upande wa Waziri wa Fedha Dk. Mgimwa aliishukuru serikali ya Japan mikopo yenye masharti nafuu kwa Tanzania ambayo imechangia kwa kiwango kikubwa kukuza maendeleo katika sekta ya barabara na kuahidi kuwa awamu ya pili ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami itatekelezwa kwa kuzingatia makubaliano.

“Napenda kukuhakikishia kuwa, serikali ya Tanzania itasimamia kwa karibu miradi yote miwili ya ujenzi wa barabara kwa ufanisi mkubwa”, Dk. Mgimwa alisisitiza.

Kwa upande wake Balozi wa Japan Masaki Okada amefurahishwa na uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi yake na Tanzania ambao umedumu kwa zaidi ya miaka hamsini sasa ikiwa ni kielelezo cha ushirikiano mzuri baina ya nchi zote mbili.

Naye Mwakilishi mkuu wa JICA nchini Tanzania Yasunori Onishi alisema kuwa sekta ya usafirishaji imekuwa moja ya maeneo muhimu katika ushirikiano kwani yanachangia ukuaji wa uchumi, ambapo alibainisha kuwa Japan kupitia JICA imeweka vipau mbele kusaidia sekta ya usafirishaji katika maeneo matatu ambayo ni, Kuimarisha miundombinu ya barabara zinazounganisha nchi nzima, pili kupunguza msongamano wa magari katika majiji kama vile Dar es Salaam na tatu ni maendeleo ya barabara vijijini.
Previous Post Next Post