ECOBANK TANZANIA KUKUZA BIASHARA KATI YA TANZANIA AND CHINA



Ecobank Tanzania Limited, ambayo ni mojawapo ya benki katika kundi la Ecobank jana imezindua rasmi kitengo cha China kiitwacho ‘China Desk’ katika hafla ya Chakula cha jioni iliyofanyika katika hoteli ya Great Wall Masaki, Dar es Salaam. Benki hiyo pia imezindua ununuzi wa moja kwa moja wa sarafu ya kiChina RMB ambayo imewalenga wafanyabiashara wanao nunua bidhaa kati ya China na Tanzania. Hafla hii iliwavutia watu wapatao 180 hasa wawekezaji wa kichina na Tanzania pamoja na wana habari.

“Kundi la Ecobank limeweka mkakati wa ushirikiano na benki ya China ili kusaidia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China. Katika mwaka uliopita, biashara kati ya nchi hizi mbili ilifikia $2.5 billioni. Sio ajabu kwamba Tanzania ilikuwa nchi ya kwanza Africa kutembelewa na Rais Mhe. Xi Jinping. Ndani ya mwaka uliopita, biashara kati ya nchi hizi mbili imeongezeka kwa asilimia 15%! Ni wakati mwafaka sisi kuzindua kitengo cha China hapa Tanzania kama ilivyo katika Ecobank nchini zingine barani Africa” Alisema Bw. Enoch Osei-Safo Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania.

Pamoja na uzoefu wa miaka 25 katika nchi 32 za Afrika, Kundi la Ecobank lina rekodi ya mafanikio katika huduma za benki kwa wafanyabiashara wa Kichina katika Afrika. Hakika, Ecobank kupitia muundo wa kimataifa wa usimamizi wa akaunti iliyopo nchini China imesaidia biashara nyingi za kiChina kuendesha biashara na uwekezaji katika nchi tofauti barani Afrika.

Katika mwaka wa 2012, Ecobank ilifungua ofisi wakilishi Beijing, ambayo inasimamia uhusiano kati ya Ecobank na biashara za kiChina barani Africa na Kampuni zilizopo Afrika zinazofanya biashara nchini China. Kupitia kitengo hicho kilichopo Beijing na mtandao wa Ecobank barani Africa, benki hii imejitokeza kama njia ya kukuza bishara kati ya China na Afrika.

Uwekezaji wa China katika Afrika umeongezeka kutoka $ 900 milioni katika mwaka 2000 hadi $ 68 bilioni katika 2010 ambayo ilisaidiwa na sera ya 'Chinafrique' inayoendeleza biashara bila vikwazo. “Uwekezaji kutoka China unazidi kukua na ofisi yetu Beijing inapokea maombi mengi sana ya ushauri wa uwekezaji Afrika.” anasema Lu Xiaoning, Meneja wa ofisi wakilishi Beijing. Hivi karibuni, Mheshimiwa Zhou Yi, mmiliki wa Hengxu ambalo ni Kundi la Makampuni iliyo na makao makuu katika Mkoa wa China Sichual, aliweka wazi mipango ya kuwekeza $ 700 milioni katika ujenzi wa hoteli ya kifahari katika mbuga ya Serengeti, Tanzania.

"Kwa wawekezaji kama Mr Yi, thamani yetu ni rahisi kwa huduma mbalimbali tunazotoa kwa soko hili la kipekee". Anasema Mr.Enoch Osei-SAFO. "Tunazidi kusaidia kukuza uwezo wa jumuiya ya biashara ya Tanzania katika kuchukua fursa zilizopo kukuza uchumi, kwa njia ya mafunzo pamoja na washirika wetu mbalimbali ikiwa ni pamoja na Benki Kuu ya Tanzania na vyombo vya habari. Hii yote inafanyika katika utekelezaji wa kauli mbiu yetu, Ecobank Inatuwezesha ampayo ina lengo la kujenga uwezo kwa Tanzania kuongeza fursa za kiuchumi, “aliongeza.

Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.ecobank.com

 Bw. Enoch, Bi. Lu Xiaoning ambaye ni Meneja wa Ofisi wakilishi ya Ecobank mjini Beijing pamoja na Bw. Erick Mushi wakifurahia habari za uendeshwaji mzuri wa biashara kati ya Ecobank Tanzania na Ofisi wakilishi Beijing.

Virginia Cortavitare na Eric Tirabassi kutoka Tanzania Invest pamoja na MkurugenziMtendaji wa Ecobank Tanzzania Bw. Enoch Osei-Safo na Mshauri wa PR nchini Daisy Mumbi wakijadiliana swala kwenye hafla ya chakula cha jioni katika hoteli ya Great Wall Masaki

Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania Bw. Enoch Osei Safo akihojiwa na wanahabari kuhusu uhusiano wa Ecobank na wafanyabiashara kati ya Tanzania na China
Previous Post Next Post