Askari wa kikosi cha usalama barabarani akijongea katika eneo la ajali mara baada ya daladala aina ya Toyota Coaster inayofanya safari zake kati ya Temeke na Posta kupitia barabara ya Kirwa lenye namba za usajili T 935 BEN kupinduka katika eneo la Mivinjeni jijini Dar es salaam kutokana na utelezi barabarani kufuatia mvua iliyonyesha asubuhi leo, hata hivyo katika ajali hiyo basi hilo halikuwa na abiria hakuna aliyepoteza maisha ila konda amepata majeraha kidogo na kupelekwa hospitali
Wananchi wakiangalia mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo leo asubuhi![](http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2013/04/33.jpg)
Breakdown akiwa tayari kwa kunyanyua gari hilo na kuliondoa katika eneo la ajali
Wafanyakazi wakifunga minyororo tayari kwa kulinyanyua gari hilo.