Bayern Munich yaandika Historia mpya .






Mabingwa wa ligi ya Ujerumani Bayern Munich wamekamilisha wiki nzuri kwao kwa kuandika historia mpya ya kuwa na bingwa mwenye idadi kubwa ya pointi kuliko wote kwenye Bundesliga .

Bayern imefikisha jumla ya pointi 83 baada ya kuifunga Freiburg 1-0 kwenye mchezo wa ligi uliopigwa mapema hii leo . Bao lililoipa Bayern ushindi lilifungwa na kiungo wa kimataifa wa Uswissi Xherdan Shaqiri ambapo limeifanya timu hiyo kufikisha pointi 84 huku ligi ikiwa imesaliwa na michezo mitatu kabla ya kumalizika .

Bayern wanamaliza wiki ambayo ilianza kwa taarifa ya kusajiliwa kwa kiungo Mrio Gotze kabla ya ushindi wa 4-0 kwenye mchezo wa nusu fainali ya ligi ya mabingwa dhidi ya Fc Barcelona ambao uliifanya Bayern kuweka mguu mmoja kwenye fainali ya michuano hiyo .

Bayern wamevunja rekodi iliyowekwa na mabingwa wa msimu uliopita Borrusia Dortmund ya pointi 83 .
Previous Post Next Post