ZIARA YA RAIS WA ZANZIBAR WILAYA YA KUSINI UNGUJA KATIKA PICHA


DSC_0007a
Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na viongozi  wakati alipowasili katika bonde la Mpunga la Muyuni Wilaya ya Kusini Unguja,kuangalia athari za kilimo cha Mpunga,akiwa katika ziara mko
a wa kusini UngujaDSC_0014a  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na viongozi  wakati alipowasili
katika bonde la Mpunga la Muyuni Wilaya ya Kusini Unguja,kuangalia
athari za kilimo cha Mpunga,akiwa katika ziara Mkoa wa Kusini Unguja.
DSC_0018a 

Rais 
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara
ya Kilimo na Maliasili   wakati alipowasili katika bonde la Mpunga la
Muyuni  Wilaya ya Kusini Unguja,kuangalia athari za kilimo cha
Mpunga,akiwa katika ziara Mkoa Kusini Unguja.
DSC_0045a

Rais wa 
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea risala ya  wananchi na Wakulima  wa
Muyuni,kutoka wa  Marium Mwinyi, alipofika katika shehia hiyo
kuangalia athari za mpunga uliopata matatizo ya kuungua na jua
kali,akiwa katika ziara ya Mkoa wa Kusini Unguja jana,
DSC_0053a

Rais wa 
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali
Mohamed Shein,akizungumza na  Wananchi na Wakulima  wa
Muyuni,alipofika katika shehia hiyo kuangalia athari za Kilimo cha
Mpunga uliopata matatizo ya kuungua na jua kali,akiwa katika ziara ya
Mkoa wa Kusini Unguja jana,IMG_6621a

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,akipanda mche wa mnazi mbele ya jengo la Jumuiya
ya Tuishi la vikundi vya ushirika vya Akina mama wa  Jambiani Mbuyuni
Shehia ya Kibigija, alipofika kukagua ujenzi wa Jengo la jumuiya
hiyo,akiwa katika ziara ya Mkoa wa Kusini Unguja jana.
IMG_6695a

Mbunge 
wa Jimbo la Muyuni CCM,pia Naibu Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimatifa  Mahadhi Juma Maalim,alipokuwa akitoa
tamko la mchango wake wa Shilingi Millioni mbili za Kitanzania,wakati
wa Harambee ya kukamilisha Ujenzi wa jengo la Jumuiya ya Tuishi
Jambiani Mbuyuni Shehia ya Kibigija, katika  ziara ya Rais , Mkoa wa
Kusini Unguja jana. IMG_6702a 

Afisa Tawala wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi
Ayoub  Mohamed  Mahmoud,akimkabidhi Fedha Dola za Kimarekani Mia tatu,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,wakati  wa harambee ya kuchangia Ujenzi wa Jengo la  Jumuiya ya
Tuishi Jambiani Mbuyuni Shehia ya Kibigija,aliyoiitisha katika   ziara
ya Mkoa wa Kusini Unguja jana.IMG_6711a

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein, alipokuwa akitoa idadi ya fedha zilizochangwa
wakati wa harambee kukamilisha ujenzi wa jengo la Jumuiya ya Tuishi
Jambiani Mbuyuni Shehia ya Kibigija,alipofika kuangalia maendeleo ya
Ujenzi wa Jengo hilo jana, akiwa katika ziara ya Mkoa wa Kusini Unguja
jana,ilifikia shilingi za Kitanzania Milioni ishirini na tano,laki
tatu na arubaini na sita elfu. 
Previous Post Next Post