TANZANIA NA DENMARK ZASAINI MAKUBALIANO YA USAFIRISHWAJI WA WATUHUMIWA WA VITENDO VYA UHARAMIA BAHARI YA HINDI.


    



SERIKALI  ya Tanzania ikishirikiana na serikali ya Kifalme ya Denmark imesaini mkataba wa makubaliano ya  ushirikiano wa usafirishwaji wa washukiwa wa uharamia pamoja na wezi wakutumia silaha watakaokamatwa na majeshi ya Denmark kwenda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni ikulu jijini Dar es salaam, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete amesema kuwa mkataba huo ni mwendelezo wa ushirikiano mzuri  kati ya Denmark na Tanzania.
Ameeleza kuwa Denmak imekuwa na historia nzuri ya ushirikiano na Tanzania, kwa miaka takribani 50 imesaidia miradi ya maendeleo pamoja na misaada ya kimaendeleo .
“Mkataba huu wa ushirikiano wa usafirishwaji maharamia mpaka Tanzania utasaidia utasaidia kukabiliana na kupunguza uharamia katika bahari ya Hindi.Alisema Rais Kikwete.
Aidha mkataba huo unairuhusu Tanzania kukubali kupokea washukiwa wa uharamia waliokamatwa na majeshi ya Denmark ili kufikishwa kwenye vyombo vya dola vyenye mamlaka na uwezo wakusikiliza kesi hizo bila upendeleo au uonevu.
Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Denmark Bi. Hellen Schmidt amesema Denmark imechukua hatua kupinga uharamia ikishirikiana na Tanzania kama sehemu ya kuendeleza  ushirikiano wake na  Tanzania.
“Tanzania ni miongoni mwa nchi chache barani Afrika ambazo hazijakumbwa na vita vya wenyewe kwa wenye,hivyo Denmark inafurahi kuwa na uhusiano mzuri na nchi hii pamoja na kuisaidia kupingana na tatizo hilo.”Alisema Waziri mkuu Schmidt.
Previous Post Next Post