RAIS KIKWETE ATEMBELEA MAJERUHI WALIOUMIA KATIKA GHOROFA LILILOPOROMOKA DAR ES SALAAM


Picture
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakimpa pole Bw. Yusuf Abdallah katika wodi ya Sewa Haji. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Mhe. Hawa Ghasia. (picha: Ikulu)
Picture
Rais Kikwete na Mama Salma katika wodi ya Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam wakimpa pole kijana Mohamed Ally Dhamji ambaye ni miongoni mwa majeruhi walionusurika katika jengo lililoporomoka katikati ya jiji Ijumaa, Machi 29, 2013 
Picture
Rais Kikwete na Mke wake Mama Salma wakiwa katika wodi ya Sewa Haji ya Taasisi ya Mifupa ya MOI, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam leo Machi 31, 2013 wakimjulia hali na kumpa pole Bw. Selemani Saidi. Kushoto mwenye suti nyeusi ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Raymond Mushi. Kulia ni Daktari C.N. Mcharo wa Taasisi ya Mifupa ya MOI.

Previous Post Next Post

Popular Items