


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali pamoja na kamati ya harambee ya ujenzi wa kanisa jipya la Kigurunyembe katika ukumbi wa Bwalo la Maafisa la Magadu mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhi kwa watawa keki maalumu iliyopigwa mnada na kununuliwa kwa zaidi ya shilingi milioni moja. Aliitoa keki hiyo kama zawadi kwa watoto yatima wanaolelewa na watawa hao

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude wakipokea keki maalumu iliyopigwa mnada na kununuliwa kwa zaidi ya shilingi milioni moja

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude wakiongea wakati wa harambee hiyo.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisimamia harambee ya ujenzi wa kanisa jipya la Kigurunyembe iliyofanyika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Magadu mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013. Kuume kwake ni Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa harambee ya ujenzi wa kanisa jipya la Kigurunyembe iliyofanyika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Magadu mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013.