POLISI MKOA WA KINONDONI YAKAMATA MAJAMBAZI SUGU 21 HUKU WANANCHI WENYE HASIRA KALI WAKIUWA JAMBAZI LINGINE SUGU.


Na.Mo Bongo 61 Team
Jeshi la Polisi mkoa wa Kinondoni Jijini Dar es Salaam limefanikiwa kuwakamata majambazi sugu 21 kufuatia doria na misako mikali inayoendelea kufanyika katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kinondoni.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Charles Kenyela (Pichani)  amesema kumatwa kwa majambazi hayo kunatokana na ushirikiano mzuri baina ya wananchi na Jeshi la Polisi kwa njia ya kutoa taarifa zenye uhakika kuhusu uhalifu na wahalifu kwenye maeneo yao.
Katika tukio jingine Kamanda Kenyela amesema jambazi sugu ajulikanaye kwa jina la Omary Said mwenye umri wa miaka 37 mkazi wa Tabata Aroma amefariki dunia kufuatia kipigo kikali alichokipata kutoka kwa wananchi wenye hasira kali baada ya yeye na wenzake watatu waliotoroka baada ya tukio la kumvamia Abdulrahaman Mohamed na kumpora pesa taslimu Tshs. 14,000,000/= zilizokuwa kwenye mfuko wa Rambo.
Aidha Jeshi hilo la Polisi Mkoani Kinondoni huko Kimara Temboni limefanikiwa kukamata silaha moja aina ya S/Gun yenye namba T 23269 na risasi 20 zilizokuwa kwenye mfuko wa Rambo baada ya majambazi wawili waliokuwa wanajiandaa kwenda kufanya uhalifu maeneo ya Kimara Temboni kuwa walikuwa wanafuatiliwa na askari na hatimaye kuamua kuitupa silaha hiyo na risasi zake.

Previous Post Next Post