Ni idadi ndogo ya Watanzania waliofanikiwa kununua na kuvitumia vinga’muzi toka mfumo wa digital uanze kutumika Tanzania lakini nilikua sijawahi kupata ni asilimia ngapi ya watu ambao hawatazami Tv kutokana na kukosa vinga’muzi.
Taarifa imenifikia kwamba utafiti wa haraka uliofanywa na umoja wa wamiliki wa vyombo vya habari MOAT umeonyesha kwamba kwa Dar es salaam pekee, ni zaidi ya asilimia 75 ya Watanzania haitazami channel za TV za nyumbani toka kuzimwa kwa mitambo ya analog ndio maana umoja huo bado umeendelea na msimamo wa kuitaka serikali kuangalia upya uwezekano wa kurudisha matangazo ya analog kwanza.
Namkariri mwenyekiti wa MOAT Reginald Mengi akisema “Watanzania wapewe muda kujiandaa ili kutoka analog kwenda digital ifanyike vizuri na kwa mafanikio makubwa, pendekezo letu lilikua ni kwamba analog na digital ziende sambamba mpaka tufike mahali tuone kwamba watu wengi kama sio wote wana vyombo vya kuwawezesha kwenda digital, hilo lifanyike kabla ya tarehe 17 june 2015 ambayo ndio siku ya mwisho ya kutumia analog”