Mwili wa marehemu Mwalimu Casto Sote Kawamba aliyepigwa risasi na Askari wa Jeshi la Polisi
ASKARI wa Jeshi la Polisi amemuuwa Mwalimu wa Shule ya Sekondari Kitulo Wilayani Mkete kwa kumpiga risasi mgongoni kwa madai kwamba mwalimu huyo alikuwa akiendesha Pikipiki bila kuvaa Helment (Kofia ya kuendeshea Pikipiki).
Akizungumza na Habarimpya.com kwanjia ya simu Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Makete Peter Kaiza alimtaja marehemu kuwa ni casto sote kawamba na kusema kwamba tukio hilo lilitokea karibu na Benki ya NMB tawi la Makete.
"Mwalimu huyo alikuwa anakwenda kupata huduma za kibenki kupitia mashine ya kutolea pesa ya ATM akiwa na pikipiki ndipo alipo amuliwa na Askari mmoja aitwae Jose Msukuma ili asimame kabla ya kukutwa na umauti huo .
"Kamanda Kaiza alisema kwamba kifo cha mwalimu huyo inadaiwa kuwa ni kutovaa kofia hiyo na baada ya kuitwa na Askari huyo alikaidi amri na kutaka kumgonga askari huyo aliye kuwa lindo.
Nae mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Makete Idd Nganya ambaye ndie mwajiri wa marehemu amesema kuwa mwili wa marehemu bado umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya makete wakati utaratibu wakusafirisha mwili huo kwenda kwao Mkoani Mbeya kwa ajili ya mazishi ukiendelea
Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Makete Dk Michael Gulaka alisema kwamba walipokea mwili wa marehemu ukiwa na majeraha ya risasi mgongoni na si kwamba marehemun alimpokea akiwa hai kama inavyodaiwa na baadhi ya watu