MUIGIZAJI WA BONGO MOVIE DEOGRATIOUS SHIJA AMEFUNGUKA JUU YA TETESI ZILIZOZAGAA MITAANI KUWA AMEFULIA NDANI YA SOKO LA BONGO MOVIE!


Shija afunguka juu ya tesesi zilizozagaa mitaaani kuwa amefulia ndani ya soko la bongomovies!

    Mwigizaji maarufu wa bongomovies nchini Deogratius Shija maarufu kama Shija, amefunguka na kuongea na mwandishi wetu juu ya habari zilizozagaa mtaani kuwa amefulia ndani ya gemu la bongo movies na kwamba hali yake kiuchumi ni mbaya hasa hasa baada ya kuonekana akiwa na ndevu nyingi sana na nywele alizoziachia bila mpangilio.
    Akizungumza nyumbani kwa Ben kinyaiya leo, Shija alisema kuwa habari hizo si za kweli, na kwamba yuko kwenye maandalizi ya ya movie yake mpya itakayoitwa "Cheti bandia" ambayo ataanza kuitengeneza wiki ijayo. Aliongeza kwa kusema kuwa ndani ya movie hiyo ambayo ataigiza kama "Main Character" au mwigizaji mkuu, atatakiwa kuwa na ndevu nyingi pamoja na nywele "rough" ili kuweza kuonesha picha halisi iliyo katika stori ya filamu hiyo.
    Shija ambaye alijipatia umaarufu kupitia filamu yake ya "Trip to London" na "Mboni Yangu" aliyoigiza pamoja na marehemu Juma Kilowoko "sajuki" amewataka mashabiki wake wakae tayari kwa ajili ya filamu yake hiyo mpya anayotarajia kuiachia katikati ya mwezi wa saba.

    Previous Post Next Post