Mwenyekiti wa SARPCCO IGP Said Mwema akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakurugenzi wa Makosa ya Jinai kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) baada ya kufungua mkutano wao wa siku mbili jijini Dar es Salaam.Mkutano huo utajadili mambo mbalimbali yanayohusu uhalifu unaovuka mipaka pamoja na kufanya Operesheni za pamoja baina ya Nchi wanachama wa umoja huo.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
Mwenyekiti wa SARPCCO IGP Said Mwema akiongea na waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa mkutano wa Wakurugenzi wa Makosa ya Jinai kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) baada ya wakati wa mkutano wa kufungua mkutano wao wa siku mbili jijini Dar es Salaam.kushoto ni DCI wa Afrika kusini Vinesh Moonoo na Mkuu wa INTERPOL Harare Chilika Simfukwe.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
Mwenyekiti wa SARPCCO IGP Said Mwema akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakurugenzi wa Makosa ya Jinai kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) pamoja na wajumbe wa Kamati tendaji za Mafunzo, Sheria na wanawake baada ya kufungua mkutano wao wa siku mbili jijini Dar es Salaam.Mkutano huo utajadili mambo mbalimbali yanayohusu uhalifu unaovuka mipaka pamoja na kufanya Operesheni za pamoja baina ya Nchi wanachama wa umoja huo.(Picha na Frank Geofray-Jeshi laPolisi)
Kaimu DCI, Naibu Kamishna wa Polisi Issaya Mngulu akiongea katika mkutano wa wakurugenzi wa Makosa ya Jinai kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).Mkutano huo wa siku mbili utajadili mambo mbalimbali yanayohusu uhalifu unaovuka mipaka pamoja na kufanya Operesheni za pamoja baina ya Nchi wanachama wa umoja huo.