MATOKEO YA MECHI ZA SIMBA NA AZAM FC JANA MARCH 3 2013 YAKO HAPA.


 Ushindi wa 5-0 dhidi ya Al Nasri Juba ya Sudan Kusini, umeipa Azam FC nafasi ya kuingia hatua ya pili ya mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuitoa timu hiyo kwa jumla ya magoli 8-1.
Azam FC inashiriki kwa mara ya kwanza mashindano hayo yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na imefanikiwa kuvuka hatua ya awali na kuingia hatua ya pili ambako zimesalia timu 36.
Azam FC imefikisha idadi hiyo ya magoli baada ya kupata ushindi wa 3-1 katika mchezo wa kwanza uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita na Jana wakacheza mechi ya pili kwenye Uwanja wa Juba Sudan Kusini na kupata ushindi wa 5-0 ambapo magoli ya leo yamefungwa na Khamis Mcha magoli matatu ‘Hat Trick’, John Bocco na Salum Abubakar wamefunga goli moja moja.
Kwa timu za Tanzania zinazoshiriki mashindano ya CAF, ni Azam FC pekee iliyosalia baada ya timu za Simba SC kutolewa na Recreativo Libolo ya Angola kwa kufungwa 4-0 leo, na Jamhuri ya Pemba nayo ikatolewa na St. George ya Ethiopia kwa jumla ya magoli 8-0.
Previous Post Next Post