KILIMANJARO TANZANIA MUSIC AWARDS YAZINDULIWA RASMI LEO

kili1
Meneja wa bia ya Kilimanjaro Bw. George Kavishe akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za TBL Masaki wakati alipozungumzia uzinduzi wa Tuzo za Kilimanjaro Music Award na kuasiniwa kawa mkataba wa udhamini wa Tuzo hizo kati ya kampuni ya TBL na
BASATA.
 kili2Kushilla Thomas Mkurugenzi wa Masoko wa TBL akibadilishana hati na Godfrey Mngereza Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA baada ya kusainiwa kwa mkataba huo, huku viongozi wengi9ne wa TBL na BASATA wakipiga makofi. kili3
Katikati ni Kushilla Thomas Mkurugenzi wa Masoko wa TBL kulia na Godfrey Mngereza Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA kushoto pamoja na Maofisa wa TBL na BASATA wakifurahia jambo mara baada ya kuzinduliwa rasmi kwa nembo  ya Kilimanjaro Music Award.
Tuzo za muziki maarufu kama Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013 zimezinduliwa leo jijini Dar es Salaam zikiwa na dhumuni kubwa la kutambua wasaniii waliopata mafanikio katika sekta ya muziki kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
George Kavishe, Meneja wa  kinywaji cha Kilimanjaro Premium Lager amesema wakati wa uzinduzi huo kuwa, “Kilimanjaro Premium Lager inajivunia kuendelea kudhamini  tuzo hizi kwa mara ya 12 sasa lengo likiwa kukuza muziki nchini Tanzania. Mchakato wa kuwapata wanamuziki bora wa mwaka unaanza leo na utamalizika tarehe 8 Juni ambapo tutakuwa na hafla ya usiku maalum wa kwa ajili ya kutangaza washindi.”
Alisema Kilimanjaro Premium  Lager imejizatiti kuendeleza tasnia ya muziki Tanzania kwa kutambua na kuwapa tuzo wasanii wenye vipaji. ‘Tunataka  wanamuziki  wetu wajisikie wanathaminiwa na kutambuliwa kwa kazi nzuri wanayoifanya  vile vile tunataka Watanzania  waweze kuthamini muziki wa nyumbani na kutambua mchango wa wanamuziki katika kuleta maendeleo ya uchumi katika nchi.
‘’Kilimanjaro Premium Lager inajivunia  kuwa sehemu ya tuzo hizi na ni matumaini yetu kua mwaka huu tukio hili litakua kubwa na zuri zaidi’’
‘’Pia tuna furaha kutangaza  kwamba BASATA imetupatia leseni ya kuendelea kudhamini tuzo hizi kwa kipindi cha miaka mingine mitano. Kusainiwa kwa mkataba mpya na BASATA ni uthibitisho wa azma kubwa tuliyonayo katika kuendeleza muziki wa Tanzania. Mkataba huu utaifanya Kilimanjaro Premium Lager kuwa mdhamini wa tuzo hizi mpaka mwaka 2018.
Previous Post Next Post