BOSCOS NTAGANDA: ASEMA ! SINA HATIA AIAMBIA MAHAKAMA YA KIMATAIFA YA UHALIFU WA KIVITA YA ICC


Kwa mara ya kwanza akipandishwa kizimbani kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC, jenerali Bosco Ntaganda amesisitiza kuwa hana hatia kuhusu tuhuma zinazomkabili mbele ya mahakama hiyo.

Congolese warlord Bosco Ntaganda looks on during his first appearance before judges at the International Criminal Court in the Hague, March 26, 2013.
Bosco Ntaganda akiwa kwenye mahakama ya ICC mara baada ya kufikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza
Akiwa amevalia suti nyeusi na akiwa amenyoa nywele zote, Bosco Ntaganda bila ya kung'ata maneno amewaambia majaji wanaosikiliza kesi yake kuwa hata hatia kwenye makosa ambayo yamewasilishwa mbele yake na ofisi ya mwendesha mashtaka.

Majaji wa mahakama hiyo wamepanga kuanza kusikiliza kesi za Ntaganda tarehe 23 ya mwezi September mwaka huu.

Bosco Ntaganda alijisalimisha Jumatatu ya wiki iliyopita kwenye ubalozi wa Marekani mjini Kigali Rwanda katika tukio ambalo liliishangaza dunia kwakuwa haikutarajiwa kwa kiongozi huyo kujisalimisha kwa hiari yale mwenyewe.

Hapo jana Ntaganda alikuwa akifanyiwa vipimo vya Afya mjini The Hague kabla ya kupandishwa kizimbani kujibu mashtaka yanayomkabili mbele ya mahakama hiyo.

Jenerali Ntaganda ambaye ni muhimu kwenye kesi hiyo kutokana na matukio yaliyotekelezwa mashariki mwa nchi hiyo, mwenyewe amekanusha uhalifu wa kivita na kushiriki vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Hii leo kiongozi uyo anatarajiwa kusomewa mashtaka yanayomkabili ili kyfahamu tuhuma zinazomkabili pamoja na majaji kutenga tarehe rasmi ya kuanza kusikilizwa kwa kesi dhidi yake.

Jenerali Ntaganda anakabiliwa na mashtaka kumi ikiwemo kuamuru Ubakaji, mauaji na kutumia watoto kwenye jeshi lake kufanya uasi mashariki mwa nchi hiyo.

Ntaganda aliyekuwa akifahamika kama "The Terminator" ameshirikiana na makundi mengi ya uasi mashariki mwa nchi hiyo licha ya kuwa aliwahi kuwa kiongozi wa juu kwenye jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC.

Previous Post Next Post