WAZANZIBARI WANAOISHI CANADA (ZANCANA) WATOA MSAADA



01(4)Mwakilishi wa Jumuiya ya Wazanzibari wanaoishi nchini Canada (ZANCANA) Bishara Al Masroori akizungumza na Wazazi wa watoto wenye ulemavu hawapo pichani katika hafla ya kukabidhi msaada kwa watu hao,kushoto ni Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Fereji huko  Makao Makuu ya Jumuiya ya watu wenye ulemavu Zanzibar Weles.
Na: Ali Issa-Maelezo Zanzibar
 Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa kwaza wa Rais Fatuma Abdullhabibu Fereji amesema kuna kila sababu za kuwasaidia Vipando watu wenye ulemavu ili
waweze kufikia katika Shughuli zao na kuungana na wenzao katika harakati za maisha.
 Hayo ameyasema leo huko Makao makuu ya Jumuiya ya watu wenye ulemavu Zanzibar Welesi alipokuwa akikabidhi Baskeli za kutembelea na vifaa mbali mbali kwa Watoto wenye ulemavu, ukiwa ni msada kutoka Jumuiya ya Wazanzibari wanaoishi nchini Kanada (ZANCANA).
 Amesema msaada wa Jumuiya ya ZANCANA unafaa kuigwa na kupigiwa mfano kwani utawawezesha Walemavu hao kukabiliana na majukumu yao ya kila siku kwa wepesi.
 Waziri Fereji amesema Walemavu wanahitaji kufanya mambo mengi ya msingi lakini kuna wakati hushindwa kutokana na ukosefu wa usafiri ikiwa ni pamoja na Baskeli na vifaa vingine vinavyoweza kuwasaidia kufanya mambo yao ipasavyo.
 “wana hitaji kwenda skuli,kutembea, kuchanganyika na wenzao,hivyo wanapo kosa vifaa kama hivi husindwa watoto wetu kuyafikia mahitaji yao muhimu hivyo msada huu ni furaha kwao na kwetu” Alisema Waziri Fereji.
 Aidha waziri huyo asema kuwa watu wenye ulemavu wanahitaji kutunzwa na kupewa haki za msingi ikiwemo elimu,afya, malazi, chakula na mengineo kitu ambacho mtu yoyote anaweza kuwawezesha watu hao si lazima wazee .
 Amesema mpaka hivi leo kuna badhi ya Wazazi wanawafungia ndani walemavu na kuwakosesha haki zao za msingi kwa madai kuwa ni hawataweza kufikia masafa ambayo huduma zinatolewa.
 Waziri Fereji amekemea tabia hiyo ya kuwafungia Walemavu na kusisitiza kuwa ulemavu si sababu ya kumkosesha mtoto elimu kwani jambo hilo liko katika milki ya Mwenyezi mungu Muumba.
 Nae Mzazi wa mtoto Mtumwa Hamad Khamis wakati akitoa shukrani alisema Msaada huo umekuja wakati muafaka kwao kutokana na kukosa Baskeli ambazo watoto wao walikuwa wanazihitaji kwa muda mrefu.
 Ameongezea kuwa mtoto wake amekuwa akipata wakati mgumu wakati wa kwenda Skuli kutokana na kukosa usafiri wa uhakika ambao unamuwezesha kwenda na kurudi Skuli anayosoma.
 Aidha mzazi huyo amegusia suala la unyanyapaa linalomkabili Mtoto wake Skulini kwao kutokana na Skuli hiyo kutokuwa ya mchanganyiko kati ya Wanafunzi Walemavu na wasiokuwa Walemavu jambo ambalo linamfanya afikirie kubadilisha Skuli.
 Jumuiya ya Wazanzibari wanaoishi nchini Kanada (ZANCANA) imetoa msaada kwa Watu wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na Bskeli za kutembelea, Viti, vifaa watoto vya kuchezea ikiwa ni jitihada za kusaidia ndugu zao wanaoishi katika mazingira magumu .
Previous Post Next Post