Taasisi ya kujitegemea inayofanya Utafiti wa masuala mbalimbali ikiwemo Utawala bora na Demokrasia hapa nchini, Synovate imetoa matokeo yake ya utafiti wake uliomalizika hivi karibuni na kubainisha vipengele muhimu ambavyo vinabashiri mustakabali wa uhai na uimara wa vyama vya siasa hapa nchini.
Utafiti huo umebainisha kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndicho chama maarufu zaidi hapa nchini kwa sasa ambapo umaarufu wake umeongezeka maradufu, utafiti huo umeonyesha kuwa zaidi ya asilimia 52 ya wananchi wote wa Tanzania wangependa kuijiunga na CCM, na hivyo kudhihirisha kuwa CCM bado ni chama Imara na kinachopendwa zaidi na watanzania walio wengi.
Rekodi hiyo mpya ya CCM inakinzana na kuviacha mbali vyama vya Upinzani ambavyo graph yao imeendelea kushuka na kupoteza umaarufu kwa kiasi kikubwa, mfano wa chama ambacho kinaongoza kambi ya Upinzani bungeni Chadema kimeshuka sana na kwamba ni asilimia 31 tu ya wananchi ndio ambao wangefikiria kujiunga na Chama hiko. Pamoja na M4C, operesheni Sangara,n.k bado hali ya chama hiko ni dhaifu mno kulingana na tafiti hizi. Hali ni mbaya zaidi kwa CUF ambayo ina asilimia 4 tu ya kuungwa mkono na watanzania.
Utafiti huo pia umebainisha kuwa kupanda kwa CCM na kuongezeka kwa umaarufu wake kunatokana na Utekelezaji wa Ilani yake kwa kasi inayoridhisha, lakini zaidi ni kutokana na Uchaguzi wake ambao umetengeneza safu mpya ambayo ni bora na imara ya Uongozi ndani ya Chama hiko kikongwe na MAARUFU duniani.
Lakini pia tafiti ya synovate imeenda mbali zaidi na kubainisha kushuka kwa Umaarufu wa Dr Slaa maarufu kama "BABU" ambapo imeelezwa kuwa ameshuka kwa asilimia 25 ambapo tafiti ya awali ilibainisha kuwa umaarufu wake ulikuwa ni kwa asilimia 42 na kwa sasa umeshuka na kubaki kwa asilimia 17 tu sawa na kushuka kwa asilimia 25.