SHEREHE YA KUTANGAZA VIVUTIO SABA VYA ASILI BARANI AFRIKA KUFANYIKA JIJINI ARUSHA TANZANIA TAREHE 11 FEBRUARY 2013


images
Sherehe za kutangaza vivutio vya asili vya bara la Afrika zinategemea kufanyika katika hoteli ya Mt Meru katika jiji la Arusha Tanzania tarehe 11 February 2013 kuanzia saa nane mchana.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Bodi ya Utalii Tanzania viongozi mbali mbali wa kitaifa na kimataifa ambao wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hiyo ambayo mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda. 

Rais wa Taasisi iliyoendesha shindano hilo la kutafuta Maajabu hayo Saba la Seven Natural Wonder Dr Philip Imler kutoka Marekani anatarajiwa kuwasili tarehe 9/2/2013 tayari kutangaza vivutio Saba vya Asili vya bara la Afrika.

Tanzania ilikuwa na vivutio vitatu vilivyoingia kwenye kinyanganyiro hicho ambavyo ni Mlima wa Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro na wanyama wanaohama wa Seregeti. Tanzania imekwisha tajwa kuwa miongoni mwa washindi ambao angalau kivutio kimoja ama zaidi Saba ya Asili Afrika.

Macho na masikio ya watanzania ni kujua ni kivutio au vivutio gani hivyo vya Tanzania vimeweza kushinda.
Previous Post Next Post