Rihanna afunguka juu ya uhusiano wake na kuamua kuweka wazi sababu zilizomfanya kumpa nafasi nyingine Chris Brown Rihanna
“Niliona ni muhimu zaidi furaha yangu bila ya kujali kito chochote “ aliliambia jarida la Rolling Stone. “Sikutaka kuacha mtazamo wa mtu yeyote hata kama ni kosa, ni kosa.”
Katika toleo hilo litakalo toka leo , Rihanna ameelezea vitu vilivyobadilika kati yao.
“Mahusiano yetu na ya zamani yanatofauti kubwa kwani sasa unatuona tunatembea sehemu mbalimbali hatuna majibizano kama zamani na cha zaidi tunaongea kuhusu mipango yetu ya maisha na tunathamini na kujua fika tunachokitaka sasa"