Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dk. Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakisalimiana na wafanyakazi wa ndege ya Rais mara baada ya kushuka kwenye ndege alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kigoma leo jioni, kwa ajili ya sherehe za miaka 36 ya CCM zitakazofanyika kesho kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho pamoja na viongozi wa vyama rafiki vya CCM kutoka nchi jirani za Burundi na DRC Congo.
Rais Jakaya Kikwete akivishwa skafumara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma leo jioni kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula na katikati ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana.
Ndege iliyomleta Rais Jakaya Kikwete ikiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma leo jioni huku ikilakiwa na wananchi waliojitokeza kumpokea Rais.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Shaaban Kirumbe Mjumbe wa NEC Wilaya ya Kigoma mjini, kulia ni Peter Selukamba Mbunge wa Jimbo la Kigoma mjini.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na wananchi mbalimbali waliojitokeza kumlaki kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Asha Baraka Mjumbe wa NEC Wilaya ya Uvinza
Rais Jakaya Kikwete akiwa amembeba mtoto Khalfan Majjid huku akizungumza naye kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma kushoto ni Baba mzazi wa mtoto huyo Majjid Khalfan.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Nape Nnauye Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Itikadi na Uenezi mara baada ya kuwasili mjini Kigoma leo.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na wananchi mbalimbali waliojitokeza kumlaki kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na wananchi mbalimbali waliojitokeza kumlaki kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma
Rais Jakaya Kikwete akiangalia vikundi vya ngoma kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma.
Wadau kutoka CCM Makao Mkuu kutoka kulia ni Lusekelo,Dr. Alice,Hassan,Jestina na Beatus wakishoo Love wakati wa mapokezi ya Rais Jakaya Kikwete katika uwanja wa ndege wa Kigoma.
Mwigulu Nchema Naibu katibu Mkuu Bara CCM akisalimiana na Asha-Rose Migiro Katibu wa Halmashauri Kuu Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wakati wa mapokezi ya Rais Jakaya Kikwete , Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Venance Mwamoto.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akijadiliana Jambo na Daniel Sanzugwako mjumbe wa NEC CCM Kasulu.
Katibu Mkuu wa CCM akimsiliza Mwanalibeneke Issa Michuzi wakati wa mapokezi ya Rais Jakaya Kikwete kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma katikati ni Nape Nnauye Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Itikadi na Uenezi.
Kushoto niJohn Bukuku Mpiganaji Kamanda wa Fullshangweblog akiwa na makamanda wenzake wakati wa mapokezi ya Rais Jakaya Kikwete kwenye uwanja wa Ndege wa Kigoma.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Rajab Mwilima kada wa CCM Kinondoni jijini Dar es salaam.