MSHAHARA WA BECKHAM PARIS ST.GERMAIN,KUSAIDIA JAMII


Mwanasoka wa Uingereza David Beckham amejiunga na klabu ya Paris St. Germain ya Ufaransa. Beckham mwenye umri wa miaka 37 amesaini mkataba wa miezi mitano kwa klabu hiyo inayomilikiwa na Qatar, Beckham amepewa jezi namba 32.
Katika kuonyesha uhamisho haukusababishwa na pesa kama kivutio David Beckham amesema mshahara wake wote wa £150,000 kwa wiki katika kipindi chote cha mkataba wake zitaenda kusaidia jamii watoto wasiojiweza huko jijini Paris Ufaransa.

Previous Post Next Post