Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL jana imemteua Dkt. Kamugisha Kazaura kuwa Afisa mtendaji mkuu wa Kampuni hiyo.
Dkt. Kazaura amechukua nafasi ya aliyekuwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Bw. Said Amir Said ambaye amestaafu hivi karibuni kwa mujibu wa sheria. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Kazaura alikuwa ni Afisa mkuu wa ufundi (CTO)wa TTCL.
Bodi ya wakurugenzi ya TTCL imewaomba wafanyakazi na menejimenti kumpa afisa Mtendaji mkuu mpya ushirikiano wa kutosha ili kuwa na mshikamamo wa pamoja ili kuleta ufanisi katika utendaji wa kazi.
Kwa kusisitiza Bodi imesema “Tufanye kazi na tusonge mbele pamoja, kama timu ililyoshikamana pamoja na iliyodhamiria kuinua utawala bora.”
Dkt. Kamugisha Kazaura alitunukiwa shahada ya Uzamili (Masters) na Uzamivu (PhD)katika fani ya Habari na mawasiliano ya simu katika chuo kikuu cha Waseda kilichopo Tokyo, Japani.